Diwani Samora wa Kijitonyama awa wa kwanza kutekeleza agizo la Katibu Mkuu CCM

Na Anneth Kagenda, Diramakini Blog

DIWANI Kata ya Kijitonyama, Dama Samora ameitisha Mkutano Mkuu Maalum wa wananchi kuelezea miradi iliyopitishwa katika bajeti ya 2021/2022 ndani ya Kata yake.
Hayo yamesemwa na Diwani huyo wakati akizungumza na DIRAMAKINI Blog jijini Dar es Salaam.

Diwani huyo ali maarufu kama Samora, amesema kuwa, mkutano huo maalum ni kufuatia agizo la Katibu Mkuu Taifa, Daniel Chongolo kwa wabunge kurudi kwa wananchi kutoa mrejesho juu ya vipaumbele vilivyopitishwa katika bajeti.

Amesema, katika mkutano huo maalum amelenga kuainisha miradi mipya minne inayotarajiwa kuanza ambapo ameutaja mradi mmoja wapo kuwa ni ule wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kijitonyama.

"Lakini pia mradi mwingine ni pamoja na ule wa madarasa sita katika Shule ya Sekondary ya Kijitonyama ambampo jengo lake litakuwa ni ghorofa,"amesema Diwani Samora.

Amesema kuwa, mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua katika Kata yake pamoja na ukarabati wa madarasa matatu katika Shule ya Msingi Mwangaza iliyopo Ali Maua.

Hata hivyo, amesema kuwa mbali na masuala yote hayo pia lengo lingine ni kuwashukuru wananchi wa kata yake.

Post a Comment

0 Comments