England yatinga Nusu Fainali Euro

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Timu ya England imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Euro 2020.
Hatua hiyo wameifikia baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ukraine usiku wa Jumamosi Uwanja wa Olimpico mjini Roma, Italia.

Mabao yamefungwa na Harry Kane mawili dakika ya nne na 50 na Harry Maguire dakika ya 46 na Jordan Henderson dakika ya 63.

Mechi hiyo inatajwa kuwa iliyotazamwa zaidi kupitia runinga, ambapo sasa England watakutana na Denmark Jumatano ijayo.

Mchezo huo ulitangulia na Denmark ambayo iliichapa Jamhuri ya Czech 2-1 Uwanja wa Bakı Olimpiya mjini Baku nchini Azerbaijan.

Mabao ya Denmark yamefungwa na Thomas Delaney dakika ya tano na Kasper Dolberg dakika ya 42, wakati la Czech limefungwa na Patrik Schick dakika ya 49.

Aidha, nusu fainali ya kwanza itazikutanisha Italia na Hispania Jumanne, wakati England na Denmark zitakutana Jumatano, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Wembley, London.

Post a Comment

0 Comments