Mtoto wa Masoud Kipanya afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mtoto wa Mtangazaji Maarufu wa Redio na Televisheni, Masoud Kipanya, Malcolm Masoud amefariki dunia.

Taarifa zilizoifikia DIRAMAKINI Blog zimeeleza kuwa, Malcolm amefariki leo.

Malcolm Ally Masoud Kipanya ni mtoto wa Sara Chande ambaye alikuwa amelala kitandani kwa miaka zaidi ya 10 akisumbuliwa na tatizo la udhaifu wa misuli unaosababisha kushindwa kufanya kitu chochote katika maisha yake.

Pamoja na hayo yote Malcolm wakati wa uhai wake alikuwa ni kijana mwenye mtazamo chanya katika maisha yake na fikra zake, kwani alikuwa akiamini kuwa kuacha kulalamika ndiyo mwanzo wa kuwa na furaha maishani.

Akiwa hajiwezi kitandani, bado alikuwa ana ndoto ambazo alitaka kuzitimiza katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wagonjwa wenzake na watu wenye ulemavu na kufungua taasisi ambayo itakuwa na msaada kwa wahitaji. Mungu ailaze roho yake mahali pema na kuwapa faraja ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki Tazama video chini kumfahamu zaidi Malcolm;

Post a Comment

0 Comments