Naibu Waziri Dkt.Mabula azindua Mradi wa Nyumba za Makazi za NHC Jangwani Sumbawanga

Na Munir Shemweta, SUMBAWANGA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezindua mradi wa nyumba 20 za makazi za Jangwani zilizopo katika manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizindua mradi wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) za Jangwani zilizopo halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa leo tarehe 19 Julai 2021.

Uzinduzi wa nyumba hizo uliogharimu bilioni 1.6 umefanyika leo tarehe 19 Julai 2021 katika manispaa ya Sumbawanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Rukwa, wabunge, madiwani na viongozi wa chama.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa nyumba hizo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula alisema, uhitaji wa nyumba nchini bado ni mkubwa lakini uwezo wa shirika la NHC peke ni mdogo ingawa kwa sasa kasi ya shirika ni kubwa katika kuendesha miradi mbalimbali.

Alisema, Wizara ya Ardhi iko tayari kuhakikisha inalifutailia shirika la Nyumba la Taifa ili liweze kutekekeza majukumu yake kama lilivyoaminiwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, NHC ni shirika pekee la umma ambalo halipati ruzuku ya kuendesha miradi yake na kukielezea kitendo hicho cha kutopewa ruzuku kama kinalifanya shirika kuhitaji na miradi mingi ili liweze kujiendesha kibiashara. 

Aliushukuru uongozi wa halmashauri ya manispaa ya sumbawanga kwa uamuzi wa kuwapangishia watumishi wake katika nyumba za NHC zilizozinduliwa na kuuelezea uamuzi huo kama motisha kwa watumishi.

”Kitendo cha kuwapangishia nyumba watumishi ni cha kijasiri na kinamfanya mtumishi asiwe na sababu ya kutokuja manispaa ya Sumbawanga kwa kuwa ana uhakika wa makazi na atafanya kazi kwa weledi,”alisema Dkt.Mabula.  

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilali alisema, pamoja na kutekelezwa na kukamilika kwa mradi wa nyumba za NHC Jangwani lakini Sumbawanga bado ina changamoto ya ujenzi wa hospitali ya wilaya aliyoieleza iko nje ya mji. 

Aliomba maeneo yanayotoa huduma kwa wananchi yaliyoko nje ya mji ni vizuri maeneo hayo yakapewa kipaumbele kwa kupatiwa miradi ya majengo ya makazi ili watumishi watakaofanya kazi maeneo hayo waweze kupanga na kufanya kazi kwa ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news