Rais Dkt.Mwinyi:Tutaendelea kushirikiana kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa ipasavyo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuhakikishia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo kuwa, ataendelea kushirikiana nae katika kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM inatekelezwa ipasavyo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi barua ya Pongezi kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Zanzibar, kama ilivyoelekezwa na Halamshauri Kuu (CC) ya CCM katika kikao cha tarehe 29 Juni 2021 kilichofanyika jijini Dodoma. Alimkabidhi barua hiyo alipokwenda Zanzibar na Sekretarieti ya CCM kujitambulisha baada ya uteuzi wao uliofanyika Aprili 30, 2021. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (aliyesimama) alipokuwa akijitambulisha na kuwatambulisha wa Wajumbe wa Sekretarieti kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu jijini Zanzibar, jana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo wakati Katibu Mkuu huyo akijitambulisha na kutambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Ikulu jijini Zanzibar, jana.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (aliyesimama) alipokuwa akiendelea kujimbulisha na kuwatambulisha wa Wajumbe wa Sekretarieti kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu jijini Zanzibar, jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Zanzibar, jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Zanzibar, jana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya UWT Queen Mlozi, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Dk. Frank Hawasi, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa UVCCM Kenan Kihongozi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme. Kutoka kulia ni Katibu wa Sekretarieti ya CCM Salum Reja, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Erasto Sima, Katibu wa NEC Oganaizesheni Moudline Castico na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi.

Rais Dkt.Mwinyi ambaye pia, ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, alimesema hayo juzi wakati alipokutana na ujumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Ikulu jijini Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi hao wakiwemo wapya pamoja na wale wa zamani kwa kuendelea kubaki katika nafasi zao na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kutekekeza majukumu ya chama na Serikali.

Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane imeshaanza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambapo hivi karibuni imepitisha Bajeti ya Kwanza ya Serikali hiyo na lililobaki hivi sasa ni kuhakikisha yale yote yaliyoahidiwa kwa wananchi yanatekelezwa.

Aidha, Dkt.Mwinyi aliwashukuru viongozi hao kwa kuja kumuona na kujitambulisha kwake na kuwaahidi kufanya kazi nao huku akiwahakikishia kwamba milango yake iko wazi na yuko tayari kukutana nao wakati wowote kwa madhumuni ya kujenga nchi sanjari na kuhakikisha CCM inaendelea kufanya vizuri zaidi.

Rais Dkt.Mwinyi aliwashukuru viongozi hao kwa kuwa karibu na Serikali zote mbili na kuahidi kufanya kazi nao ili maendeleo zaidi yaweze kupatikana.

Pia, Rais Dkt.Mwinyi aliueleza uongozi huo kwamba pale watakapokuwa tayari kuuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Serikali zote mbili wawe huru kueleza yale yote yanayopaswa kufanywa vizuri zaidi kwa lengo la kuitakia mema CCM na Serikali zake mbili.

Mapema Katibu Mkuu huyo wa CCM Taifa, Daniel Chongolo alisema kuwa, ujio wake wa kukutana na Rais Dkt. Mwinyi pamoja na ujumbe wake huo ni kuja kujitambulisha kwake ambapo pia, tayari ameshajitambulisha kwa wazee, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pamoja na kuzungumza na baadhi ya wanaCCM wa Zanzibar.

Pia, Katibu Mkuu huyo alimpongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa niaba ya Sekretarieti kwa kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi wa Zanzibar huku akitumia fursa hiyo kumkabidhi Azimio la Halmashauri Kuu ya Taifa la kumpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Sambamba na hayo, Katibu Mkuu huyo alieleza kwamba ziara yake ya hapa Zanzibar imempa mwanga mkubwa wa jinsi Serikali anayoiongoza Rais Dkt. Mwinyi inavyofanya juhudi za kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wa Zanzibar.

Pia, Katibu Chongolo alimueleza Rais Dkt.Mwinyi kwamba wazee wa CCM Zanzibar wametoa azimio la kumpongeza yeye pamoja na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Wakati huo huo, Rais Dkt.Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulikia misaada ya Kibinaadamu kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE), Sheikh Ahmad Al Nazir Al Falasi na ujumbe wake.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Mwenyekiti wa “Foundation of Humanitarian Initiative” ya UAE Bw.Ahmad Al Nazr Al Falasi alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mgeni wake Mwenyekiti wa “Foundation of Humanitarian Initiative” ya UAE Bw.Ahmad Al Nazr Al Falasi alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Katika mazungumzo yake ya taasisi hiyo, Rais Dkt. Mwinyi aliihakikishia taasisi hiyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na taasisi hiyo katika kuimarisha huduma za kijamii pamoja na zile za kimaendeleo.

Rais Dkt. Mwinyi aliipongeza taasisi hiyo kwa utayari wake wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kusaidia vifaa tiba katika Hospitali kuu za Unguja na Pemba ikiwemo Hospitali ya Mnazi Mmoja na Vitongoji Pemba.

Mapema Sheikh Ahmad Al Nazir Al Falasi alimueleza Rais Dkt. Mwinyi azma ya taasisi anayoingoza ya kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya hapa Zanzibar.

Aidha, Al Falasi alimueleza Rais Dkt. Mwinyi kwamba mbali ya kuunga mkono juhudi hizo pia, amevutiwa na mazingira ya uwekezaji katika sekta ya kilimo hapa Zanzibar na kuahidi kutekeleza azma yake hiyo.

Ujumbe huo ambao ulifuatana na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui pia, ulitarajia kutembelea kisiwani Pemba katika hospiitali ya Vitongoji, Chake Chake na Wete.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news