RC Makalla atangaza uvaaji wa barakoa Dar ni lazima

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Amos Makalla amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo kufuatia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ambapo amesema watafanya ziara za kushtukiza kwenye vituo vya daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia utekelezaji wa agizo hilo.

Aidha, RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospitalini na kuwataka wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya afya.

"Tunakulinda na wewe utulinde, vaa barakoa kwa mustakabali wa afya yako na wengine,"amesema Mkuu huyo.

Wakati huo huo, RC Makalla amewataka LATRA kusimamia level seat huku akibainisha kuwa, Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya zinapaswa kusimamia utekelezaji wa Mwongozo wa Wizara ya Afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news