RUWASA PANGANI WAELEZA MIKAKATI YA KUWAPATIA WANANCHI MAJI

Na Yusuph Mussa, Diramakini Blog

MIRADI sita yenye thamani ya sh. bilioni 2,148,851,154 itatekelezwa kwenye Wilaya ya Pangani mkoani Tanga kwa mwaka wa fedha 2020/2021, ambapo itakapokamilika itaweza kuhudumia wananchi 13,996, na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji kwenye wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo akifungua Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Watumia Maji Wilaya ya Pangani. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Pangani Hassan Nyange na kulia ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Pangani Mhandisi Rajabu Yahya. (Picha na Yusuph Mussa).

Hayo yalisemwa kwenye Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Watumiaji Maji (CBWSO's) Wilaya ya Pangani na Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wa Wilaya hiyo Mhandisi Rajabu Yahya.

Mhandisi Yahya alisema miradi hiyo inayoendelea na utekelezaji kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maji (NWF) ni ujenzi wa mradi wa maji Mbulizaga wenye thamani ya sh 596,144,811 na hadi sasa umefikia asilimia 85, na utahudumia wananchi 1,997. Ujenzi wa mradi wa maji Mikocheni wenye thamani ya sh. 454,160,237.52. Hadi sasa umefikia asilimia 80, na utahudumia wananchi 1,212.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo akifungua Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Watumia Maji Wilaya ya Pangani. (Picha na Yusuph Mussa).

"Upo ujenzi wa mradi wa maji Msaraza una thamani ya sh. milioni 214,098,699 na umefikia asilimia 60, na hadi kukamilika kwake utahudumia wananchi 5,113. Ujenzi wa mradi wa maji Ushongo sh. milioni 460,227,098 na umefikia asilimia 50, na utakapokamilka wananchi 1,250 watanufaika," amesema Mhandisi Yahya.

Lakini pia ukarabati wa mradi wa maji Kibinda (Mkwajuni) wenye thamani ya sh. milioni 77,000,000, Awamu ya Kwanza ya mradi umekamilika kwa asilimia 100, na unatoa huduma, na kwa sasa upo Awamu ya Pili, na umefikia asilimia 68, na ujenzi wa sump well unaendelea, huku wananchi 1,548 wakitarajiwa kunufaika na mradi huo. Ujenzi wa mradi wa maji Masaika wa sh. milioni 346,363,308.09 na umefikia asilimia 95, na unatoa huduma ya maji kwa wananchi 2,876.

Yahya amesema jumla ya miradi minne (4) imeweza kusanifiwa na kupatiwa vibali kwa ajili ya utekelezaji wake katika mwaka wa Fedha 2021/2022 ambayo ni mradi wa maji Mikinguni – Stahabu, Meka – Mseko, Mbulizaga kwenda Mkalamo na mradi wa maji Kwakibuyu. Na jumla ya miradi miwili ipo katika hatua ya kufanyiwa Usanifu, ambayo ni mradi wa maji Mwembeni na Mrozo.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Pangani Rajabu Yahya akitoa taarifa ya miradi ya maji. Ni kwenye Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Watumia Maji Wilaya ya Pangani. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo. (Picha na Yusuph Mussa).

Mikakati ya utatuzi wa changamoto kwa vijiji visivyo na huduma ya maji ni Kijiji cha Jaira chenye wananchi 577 na Madanga chenye wananchi 1,645, ambapo kisima kilikauka, lakini kisima kingine kinachimbwa na ukarabati mradi utagharimu sh. milioni 200 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Kijiji cha Stahabu chenye wananchi 1,844, ambapo kisima kitatumika cha kijiji cha Mikinguni, na kibali cha ujenzi wa mradi kimetolewa na sh. milioni 690 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Kijiji cha Mkwaja chenye wakazi 1,234 kuna chumvi, na upanuzi mradi wa Mikocheni kwenda Mkwaja umetengewa sh. milioni 400 kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kijiji cha Buyuni kikiwa na wananchi 206 kumeonekana kuna chumvi, lakini katika utafiti wa chanzo kumetengwa sh. milioni 40 kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kijiji cha Kirupu kuna chumvi, utafiti wa chanzo sh. milioni 40 mwaka wa fedha 2021/2022.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Watumia Maji Wilaya ya Pangani. (Picha na Yusuph Mussa).

Kijiji cha Mkalamo kikiwa na wananchi 1,018, kisima kipo, na kibali cha ujenzi kimotolewa na utekelezaji wa mradi ni sh. milioni 596,144,811 kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kijiji cha Sange kuna chumvi, na utafiti wa chanzo ni sh. milioni 40 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 . 

Kijiji cha Mivumoni (Kovukovu) kuna chumvi, utafiti wa chanzo sh. milioni 40 kwa mwaka 2021/2022 na Kijiji cha Mwembeni kisima kipo, hatua za usanifu zimeanza kwa gharama ya sh. milioni 20 mwaka wa fedha 2021/2022.

Mhandisi Yahya alisema katika Wilaya ya Pangani upatikanaji wa Maji Safi na Salama ni asilimia 75 sawa na watu 30,963 kati ya watu 41,285 waishio vijijini katika umbali usiozidi mita 400, ambapo upatikanaji wa maji unategemea chanzo cha Mto Pangani na visima virefu na vifupi. Wakati upatikanaji wa Maji Safi na Salama Pangani Mjini ni asilimia 68 sawa na watu 13,282 kati ya watu 19,533 waishio Pangani mjini.

Hata hivyo utekelezaji wa miradi ya maji Mikocheni, Mbulizaga, Msaraza, Ushongo na Masaika inayoendelea kutekelezwa itakapo kamilika ifikapo Desemba, 2021 itapelekea upatikanaji wa maji Pangani vijijini kufikia asilimia 85 sawa na watu 35,092 watakao nufaika na huduma ya maji.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Watumia Maji Wilaya ya Pangani. (Picha na Yusuph Mussa).

Vile vile katika kuhakikisha kuwa miradi yote ya maji inayokamilika inakuwa endelevu, Jumla ya vyombo vya Watoa Huduma ya Maji ( CBWSOs, COWSOs na VWC) 18 vimesajiliwa kisheria na vinaendesha miradi ya maji, ambapo CBWSOs 10 zimeweza kuhuishwa kwa kutumia sheria mpya Na.5 ya Mwaka 2019, COWSO saba zipo hatua ya Kusajiliwa kuwa CBWSO na VWC moja, Vile vile CBWSO nne mpya simesajiliwa na kuwa CBWSO..

"Changomoto ya ukosefu wa maji itatatuliwa kabisa kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa miji 28, ambapo ujenzi wake utaanza mwaka wa fedha huu 2021/2022, na Wilaya ya Pangani ni miongoni mwa wilaya zitakazo nufaika na mradi huu. Kukamilika kwa miradi hii ifikapo Desemba, 2021 itafanya upatikanaji wa huduma ya maji Pangani kwa vijijini kufikia asilimia 85 sawa na watu 35,092 watakao nufaika na huduma ya maji," alisema Yahya.

Post a Comment

0 Comments