Simba SC yatwaa ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara


Wekundu wa Msimbazi, Simba SC ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa nne mfululizo.

Ni baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga usiku huu dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashuri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na washambuliaji, Nahodha John Raphael Bocco dakika ya 14 na Mkongo, Chris Kope Mutshimba Mugalu dakika ya 23.

Simba SC imefikisha alama 79 baada ya mechi 32, tisa zaidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC kuelekea mechi mbili za mwisho za msimu.

Post a Comment

0 Comments