Sophia John Nyerere afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mjukuu wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Sophia John Nyerere amefariki dunia.
Hayati Baba wa Taifa akiwa na Sophia wakati wa uhai wake.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Mheshimiwa Makongoro amesema, Sophia ni mtoto wa kaka yake marehemu, John Nyerere.

"Sophia alikuwa na familia, hivyo tutakaa pamoja kufahamu namna mazishi yatakavyofanyika," amesema Makongoro.

Wakati huo huo, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amebainisha haya;
Umeondoka Dada yangu Sophia John Nyerere, kwa heri Dada, tutaonana baadaye.

Umeniachia mawazo mazuri ya maendeleo ambayo ulitamani tufanye pamoja. Daima nitakumbuka maneno yako haya “Kaka Msigwa, tuna mambo mengi ya kufanya kwa ajili yetu na jamii nzima, kubaki masikini wakati tuna uwezo wa kufanya kazi ni kujitakia” Nasikitika hatukufanikiwa kuyatekeleza mawazo haya.

Hakika uliyaishi mawazo ya Babu yako na Baba wa Taifa letu Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Nakuombea Mwenyezi Mungu akuweke mahali pema peponi, nampa pole Bibi yako, Mama Maria Nyerere na wanafamilia wote. Mwenyezi Mungu awatie nguvu, uvumilivu na ustahimilivu.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina. 

Post a Comment

0 Comments