Ugomvi wa wafugaji na wakulima waibuka Namtumbo, avunjwa mkono kwa mkuki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mkulima Akida Mohamedi Pili (32) wa Kijiji cha Mtakuja wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma amenusurika kifo baada ya kukutana na mfugaji akiwa na mifugo yake akilisha mpunga aliokuwa akivuna katika majaruba yake.
Akida alidai akiwa yeye, mke wake na vibarua wawili waliokuja kumsaidia kuvuna mpunga eneo la Ligalango lililopo kijiji cha Njomlole yalipo majaruba yake alishangaa mfugaji mmoja ambaye hakujulikana jina lake aliingiza mifugo katika jaruba lake na wakaanza kula mpunga na kuukanyaga kanyaga mpunga ambao ulikuwa bado kupigwa.

Bwana akida hakuweza kuvumilia kitendo hicho, akaanza kurushiana maneno na mfugaji huyo bila mafanikio na kuamua kupiga simu kwa mtendaji wa kijiji cha Njomlole kuhitaji msaada wa kiserikali na wakati anapiga simu kueleza tukio hilo, mfugaji akamwambia, "nitakuua wakija kunikamata mimi".

Akida alidai msaada kutoka serikali ya kijiji cha Njomlole ulishindikana, lakini mtendaji wa kijiji cha Njomlole alimwambia awasiliane na mtendaji wa kijiji cha Mtakuja ashughulikie hilo kwa kuwa yaliyopo majaruba hayo ni jirani na kijiji cha Mtakuja.

Mtendaji wa kijiji cha Mtakuja, Bwana Kaisi Mbawala alikiri kupigiwa simu na mtendaji wa kijiji cha Njomloe kumweleza tukio hilo pamoja na mkulima mwenyewe pia kumweleza tukio hilo na kuhitaji msaada wa kisheria na ofisi yake ilituma mgambo saba wakiwemo wafugaji wenzake na walipofika eneo la tukio hawakumkuta alikuwa ameondoa mifugo yake na tayari alishamdhuru kijana Akida kwa mkuki.

Kaisi aliongeza kuwa mgambo hawakumkuta akida kwa kuwa alisha umizwa na mfugaji huyo na kuchukuliwa na mwendesha pikipiki aitwaye Salumu Taji mwenyeji wa kijiji cha mkongo aliyefika dimbeni hapo kuchukua mpunga kwa ndugu yake akalazimika kuacha kuchukua mpunga na kumchukua majeruhi na kumfikisha polisi kituo cha mkongo na kisha kumfikisha kituo cha afya mkongo

Ngika Rukomya mmoja ya wafugaji waliotumwa na ofisi ya kijiji kwenda kumkamata mfugaji aliyefanya uhalifu huo alidai kabla ya kwenda kwa mhalifu walijadiliana kuwa wasiende wote kwa pamoja kwa kuwa mtu huyo sio mzuri na kwa kuwa kitendo alichokifanya lazima atakuwa amejipanga kwa uhalifu mkubwa, hivyo akawaomba mgambo wenzake wabaki sehemu yeye aende akaangalie mazingira yalivyo kabla ya kwenda wote pale.

Rukonya alipofika katika kambi ya mtuhumiwa huyo akamuuliza unafika kufanya nini huku kukiwa na vijana wanne waliojiandaa kufanya matukio mabaya, lakini bwana Akada amefika kuangalia ndama wake kama wameungana na kundi la ng'ombe wako huku wakijua ni mfugaji mwenzao hawakufanya lolote.

Rukomya alitazama tazama kama ndama wa mfugaji yule na kisha kumwambia mfugaji yule kuwa ndama wake hawapo pale, lakini pamoja na hilo akampa angalizo kuwa, "kama ulikuja kunipeleleza mimi hakikisha nikikamatwa mimi kupelekwa polisi wewe hutabaki salama," alimwambia Rukomya.

Bwana Rukomya alirudi mpaka kwa mgambo wenzake na kuwaambia hali iliyopo sio nzuri cha msingi warudishe majibu ofisi ya kijiji kuhitaji nguvu zaidi kwa kuwa mfugaji mwenzake huyo amejiandaa kwa mapambano makali.

Mgambo Tarime Lukwaja,Kenya Lugweza,Maula Msanja ,Mabula Masanja Gaudensi Mvula,Joakimu Nchimbi na Ngika Rukomya waliripoti ofisi ya mtendaji wa kijiji cha mtakuja kuwa uwezo wa wao kumkamata mtuhumiwa ni mdogo kwa kuwa amejipanga kwa kufanya mauaji makubwa.

Baba mzazi wa Akida Pili aitwaye Mohamedi Akida alisema alisikia kelele kwenye majaruba ya mwanae akaamua kuja kutazama kuna nini na alipofika alikutana na kundi la mifugo la mfugaji na kumsaidia kijana wake kupambana na mfugaji huyo na aliposogea kusaidiana na kijana wake kumshamabulia kwa maneno mfugaji huyo akiwa na mikuki alichomoa mkuki kwa lengo la kumdhuru Mohamedi Akida na kwa bahati nzuri mkuki ule aliukwepa na ulipita sentimita chache kutoka alipo yeye.

Kwa mujibu wa mzee Akida mwenyewe alisema kuwa baada ya kumkosa ule mshale akagundua yule mfugaji hana nia njema akamhimiza mwanae kuendelea kumpigia simu mtendaji wa Kijiji cha Mtakuja ili mgambo wale wafike haraka wamkamate huku vibarua na mke wake walikimbia shambani hapo.

Ofisi ya mtendaji wa kijiji ilidai imeandika barua kupeleka kituo cha polisi Mkongo kuijulisha ofisi hiyo kuhitaji msaada wa polisi ili kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu huku mkulima aliyenusurika kifo alifikishwa Hospitali ya Rufaa Songea ambapo amepatiwa matibabu na kufungwa mhogo katika mkono wake uliovunjwa na mfugaji kwa mkuki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news