Wakesha mbugani usiku wakisaka kinyesi cha tembo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Katika Kitongoji cha Sengasenga kilichopo Kijiji cha Musimi Kata ya Sepuka Wilaya ya Ikungi mkoani Singida baadhi ya wananchi wamekesha siku nzima usiku wakiwa mbugani wakivizia wapate kinyesi cha tembo wakidai ni dili mashambani.

Sambamba na dawa ya watoto wadogo baada ya tembo wawili kuingia na kuonekene kwenye eneo lao saa 2:00 asubuhi.
DIRAMAKINI Blog katika maeneo hayo imeelezwa kuwa,walipofikia wanyama hao watu wengi walijitokeza kutaka kuwafahamu tembo walivyo huku wengine wakipiga picha kwa kutumia simu zao na kamera na wengine walifika kuwaona tembo hao kwa nia ya kusaka kinyesi chake.

Pia walidai yanatumika mashambani na mchanganyiko wake ni dawa ya kutibu degedege kwa watoto wadogo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sengasenga, Saidi Omari akizungumza na DIRAMAKINI Blog amesema, tembo hao walionekana majira ya asubuhi katika eneo hilo wakitokea Mashariki wakielekea Magharibi mwa kitongoji hicho

Omari amesema, tembo hao walipita karibu na nyumbani kwake umbali wa mita 100 saa 2:00 asubuhi wakielekea Magharibi ndipo watu wakawapigia kelele wakageuza mwelekeo wakaelekea Kusini mbugani na walikaa huko siku nzima.

Wakazi wa Sengasenga wamesema, mwaka huu ni wa neema kwao kutembelewa na wageni hao muhimu wakitabiri kupata mavuno mengi kwenye mashamba yao watakayolima.

Athumani Nkau ameieleza DIRAMAKINI Blog kuwa, hiyo ni baraka na pia mvua itakuwa nzuri, "hata hivyo hawajaleta madhara yeyote kwenye mashamba ya watu na kwa watu wengine,".

DIRAMAKINI Blog ilielezwa kuwa, huenda tembo hao kutoka Hifadhi ya Pori la Mgori walikuwa wanaenda kwenye Hifadhi ya Pori la Rungwe kupitia hifadhi ndogo ya Minyuge mjini hapa.

Je? kinyesi cha tembo ni dawa

Katika mahojiano maalum na DIRAMAKINI Blog, mmoja wa wataalam wa tiba asili ameeleza kuwa, kuna ukweli wa asilimia 100 kwamba, kinyesi hicho kikikauka ni tiba tosha.

"Ndiyo, tembo akishakunywa yale mavi (kinyesi) yakikauka ni dawa nzuri kwa wenye degedege. Unachopaswa kukifanya baada ya kukauka, chukua mvuje, mavi ya tembo, majani ya vitunguu saumu yaliyomenywa. Mfushe kwa siku tatu mfululizo mara mbili kwa siku mtoto atakaa sawa.

"Mtoto anayelia usiku au anastuka akiwa usingizini unamfukiza kabla ya kulala na pia ukiwa una maumivu ya kichwa au kipandauso kinakusumbua unajifukiza au unanusa ule moshi, fusho hilo pia huweza kukata damu puani.

"Vivyo hivyo,mavi ya tembo hutumika kutengenenzewa fusho chafu hutegemea aina ya jini,"amebainisha Mtaalamu huyo wa tiba asili katika mahojiano na DIRAMAKINI Blog.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news