WANANCHI WASHANGILIA UJIO WA KITUO CHA AFYA NGWELO

Na Yusuph Mussa, Lushoto

WANANCHI wa Kijiji cha Kigulunde, Kata ya Ngwelo, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, wamepokea kwa shangwe ujenzi wa Kituo cha Afya Ngwelo, kwani itakuwa ni mkombozi kwao, badala ya kufuata huduma hiyo mbali kwenye Kituo cha Afya Mlola ama Mlalo.
Jengo la huduma ya Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Kituo cha Afya Ngwelo, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Jengo hili ambalo lilianza kama Zahanati ya Kijiji cha Kigulunde, Kata ya Ngwelo, ambalo lilitengewa sh. milioni 22 hadi kukamilika kwake, sasa litakuwa OPD, huku ndani yake kukiwa na vyumba vya huduma nyingine. Ni baada ya Serikali kutenga sh. milioni 250 kwa ajili ya Kituo cha Afya Ngwelo. Hivyo kitaongezwa majengo mengine manne (4). (Picha na Yusuph Mussa).

Ni baada ya Mbunge wa Jimbo la Lushoto Shaaban Shekilindi maarufu 'Bosnia' kufanya mkutano wa hadhara Julai 25, 2021 kwenye Kijiji cha Kigulunde na baadae kuombwa ufafanuzi na wananchi kutaka kujua kituo hicho kitajengwa wapi kati ya Kijiji cha Kigulunde ama Kihitu.

Shekilindi alisema mchakato wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ngwelo ulifanyika tangu mwaka 2016, na kupitia Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) chini ya Mwenyekiti aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngwelo Isack Singano, maamuzi yalifikiwa kijengwe Kijiji cha Kigulunde, hivyo Mbunge anaheshimu maamuzi ya wananchi.

"Mimi naheshimu mawazo ya wananchi kwa kuwa wao walikaa kwenye kikao cha WDC chini ya Diwani mzee Isack Singano, na wakakubaliana. Mimi jukumu langu lilikuwa kusukuma ili mambo yaende. Na kweli Serikali ni sikivu na imetupatia sh. milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa OPD (jengo la wagonjwa wa nje) sh. milioni 22. Nashukuru nguvu za wananchi zimetumika na jengo limekamilika, bado choo na jiko la kuchomea taka.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi maarufu kama Bosnia akikagua jengo la huduma ya Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Kituo cha Afya Ngwelo, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Jengo hilo ambalo lilianza kama Zahanati ya Kijiji cha Kigulunde, Kata ya Ngwelo, ambalo lilitengewa sh. milioni 22 hadi kukamilika kwake, sasa litakuwa OPD, huku ndani yake kukiwa na vyumba vya huduma nyingine. Ni baada ya Serikali kutenga sh. milioni 250 kwa ajili ya Kituo cha Afya Ngwelo. Hivyo kitaongezwa majengo mengine manne (4). Wa pili kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngwelo Yosse Shekaholwe. (Picha na Yusuph Mussa). 

"Na hata Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto (Ikupa Mwasyoge) aliwaeleza baada ya jengo hili, kutajengwa majengo mengine manne (4), hivyo niwaombe wananchi wangu, sh. milioni 250 ni kidogo, mnatakiwa kwa umoja wenu wananchi wote wa kata Ngwelo mjitoe kwa moyo kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya. Mimi nipo pamoja nanyi kuhakikisha azma yetu ya kupata kituo cha afya inakamilika," alisema Shekilindi.

Shekilindi aliwahakikishia wananchi wa kata hiyo kupata maji ya uhakika, ambapo mradi wa maji wa sh. milioni 500 unajengwa kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa kata hiyo yenye vijiji viwili, na ujenzi wake ambao upo chini ya Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umeanza.

"Baada ya Kata ya Ngwelo na Kilole kutokuwepo kwenye mradi mkubwa wa maji wa kata 13 kati ya kata 15 za Jimbo la Lushoto, tulihakikisha kata hizi mbili nazo zinapata maji. Hivyo mradi wenu wa maji wa sh. milioni 500 kwenye Kata ya Ngwelo unaendelea vizuri. Hivyo mtapata maji ya uhakika," alisema Shekilindi.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi maarufu kama Bosnia (wa pili kushoto) akipokea taarifa kutoka kwa Ofisa Mtendaji Kata ya Ngwelo Paulina Dhahabu (kulia). Ni baada ya kufika na kukagua jengo la huduma ya Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Kituo cha Afya Ngwelo, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Jengo hilo ambalo lilianza kama Zahanati ya Kijiji cha Kigulunde, Kata ya Ngwelo, ambalo lilitengewa sh. milioni 22 hadi kukamilika kwake, sasa litakuwa OPD, huku ndani yake kukiwa na vyumba vya huduma nyingine. Ni baada ya Serikali kutenga sh. milioni 250 kwa ajili ya Kituo cha Afya Ngwelo. Hivyo kitaongezwa majengo mengine manne (4). Wa pili kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngwelo Yosse Shekaholwe. (Picha na Yusuph Mussa).

Shekilindi alisema, pamoja na mradi wa majisafi, pia kutajengwa mabwawa mawili hadi matatu kwenye kata hiyo ili kuwasaidia wananchi kwa maji ya kilimo cha umwagiliaji, lakini pia kuwezesha wananchi kuyatumia kwa kunywa pindi inapobidi. Hivyo mipango ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuwasaidia wananchi kuondokana na kero mbalimbali.

Aliwataka wananchi kujitokeza kufanya kazi kwa miradi ya Serikali inayopelekwa kwenye kata hiyo ikiwemo ujenzi wa mradi wa maji ambao umeanza, lakini pia na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe ya kutoka Mlalo- Ngwelo- Mlola- Makanya- Milingano- Mashewa wa kilomita 70, huku Serikali ikiwa imetenga sh. bilioni 3.5, hivyo wananchi waweze kuuchangamkia.

Awali, mwananchi Karim Majata alitaka kujua Kituo cha Afya Ngwelo kitajengwa wapi, na lini kitatoa huduma, huku Ali Paula akitaka kujua ni lini vikundi 30 vilivyosajiliwa ili kupata kazi za muda (vibarua) kwa kazi kutoka serikalini, vitaanza kupata kazi hizo.
Wananchi wa Kijiji cha Kigulunde wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi maarufu kama Bosnia (hayupo pichani) ambaye alifika kukagua jengo la huduma ya Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Kituo cha Afya Ngwelo, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Jengo hilo ambalo lilianza kama Zahanati ya Kijiji cha Kigulunde, Kata ya Ngwelo, ambalo lilitengewa sh. milioni 22 hadi kukamilika kwake, sasa litakuwa OPD, huku ndani yake kukiwa na vyumba vya huduma nyingine. Ni baada ya Serikali kutenga sh. milioni 250 kwa ajili ya Kituo cha Afya Ngwelo. Hivyo kitaongezwa majengo mengine manne (4). Wa pili kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngwelo Yosse Shekaholwe. (Picha na Yusuph Mussa).
Wananchi wa Kijiji cha Kigulunde wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi maarufu kama Bosnia (hayupo pichani) ambaye alifika kukagua jengo la huduma ya Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Kituo cha Afya Ngwelo, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Jengo hilo ambalo lilianza kama Zahanati ya Kijiji cha Kigulunde, Kata ya Ngwelo, ambalo lilitengewa sh. milioni 22 hadi kukamilika kwake, sasa litakuwa OPD, huku ndani yake kukiwa na vyumba vya huduma nyingine. Ni baada ya Serikali kutenga sh. milioni 250 kwa ajili ya Kituo cha Afya Ngwelo. Hivyo kitaongezwa majengo mengine manne (4). Wa pili kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngwelo Yosse Shekaholwe. (Picha na Yusuph Mussa).

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ngwelo Paulina Dhahabu alisema baadhi ya kazi za Serikali zimeanza kufanyika, lakini pamoja na kuwahamasisha vijana wajitokeze kwa wingi kwenye kazi hizo imekuwa ni shida. Mfano Mradi wa maji Ngwelo ambao chanzo cha maji (Intake) kimeshajengwa, na sasa hivi wanachimba mashimo kwa ajili ya tenki la Kijiji cha Kigulunde, na mitaro ya kupeleka mabomba Kijiji cha Kigulunde, mpaka baadhi ya mabomba yameanza kutandazwa.

"Vijana wa Kata ya Ngwelo wamekuwa wagumu kujitokeza kwenye hizi kazi za Serikali, ambapo wenzao wa Kata ya Kilole ndiyo wanajitokeza kwa wingi, na kila wiki wanalipwa," alisema Dhahabu.

Diwani wa Kata ya Ngwelo Yosse Shekaholwe aliwaeleza wananchi wamuunge mkono Mbunge kufanikisha miradi hiyo, kwani sio kila Mbunge anapata miradi mingi kama hiyo, hivyo inatakiwa kujitoa kwa hali na mali ili kufanikisha miradi hiyo kwa kufanya msalagambo, lakini na kwa ile ambayo wanalipwa, pia vijana waweze kuchangamkia, kwani mtu akisema asubiri ajira za kutumia vyeti hawezi kupata kirahisi kwa sasa, na hiyo ni dunia nzima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news