Wapigwa shoti ya umeme wakati wakibomoa vibanda vya Machinga

Na Mwananchi Digital

Wafanyakazi wanne wa kampuni ya Khimji wamejeruhiwa baada ya kupigwa na shoti ya umeme baada ya winchi walilokuwa wamepanda kugusa nyaya za nishati hiyo.
Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Julai Mosi, 2021 katika mtaa wa Kirumba inakofanyika shughuli ya kubomoa vibanda vya wamachinga wanaodaiwa kuvamia eneo.

Shuhuda wa tukio hilo, Imani Japhet amesema winchi hilo lililokuwa limebeba kontena la mmoja wa wafanyabiashara hao kwa lengo la kulihamishia sehemu nyingine liligusa nyaya hizo.

"Nilikuwa karibu ya gari ghafla nikaona shoti imekamata gari hawa wafanyakazi walikuwa juu ya gari wakapigwa nakuja kushtuka wamedondoka chini," amesema Japhet.

Mwananchi Digital ilifika eneo hilo na kukuta watu hao wakiondolewa na kupelekwa hospitali.

Post a Comment

0 Comments