Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda awaasa vijana kuchangamkia fursa ya kilimo

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mizengo Peter Pinda amewataka vijana wote nchini kuchangamkia fursa ya kilimo chenye tija (kilimo sayansi) ili kujikwamua kiuchumi badala ya kukaa mitaani bila kazi ya kufanya.
Mheshimiwa Pinda ameyasema hayo jijini hapa wakati alipokuwa akizindua wiki ya Kampuni ya PASS (Private Agricultural Sector Support) Trust ambayo inajihusisha kuwasaidia na kuwawezesha wakulima kupata mikopo kutoka kwenye benki kwa ajili ya kuendeleza kilimo.

Amesema, vijana ambao wamemaliza vyuo na wengine walioko mtaani wanayo fursa kubwa kujiajiri kwa baishara ya kilimo ambayo imewatoa wengi badala ya kusubiri ajira Serikalini.

Aidha, ameitaka kampuni hiyo wanayo nafasi ya kutafuta mashamba na kuajiri vikundi vya vijana kwa ajili ya kulima zabibu na mazao mengine, ambao watakuwa chini yao na kusaidiwa katika kusimamia kilimo na kikakua zaidi.

"Niwapongeze sana PASS kwa kuanza kuwasaidia wananchi ila niwaeleze ukweli watu hawajaijua kampuni yenu katika kuendeleza Sekta ya Kilimo na wananchi watafurahia sana kwani mkiwafikia hasa walioko vijijini kwani mmeaminika na mabenki,"amesema Pinda.

Amesema, wananchi wana changamoto kubwa ya viwanda vya kuzalisha mvinyo hivyo ni fursa kwa uongozi wa mkoa kuhakikisha wanashirikiana na kampuni hiyo ya PASS kujua namna ya kuanzisha viwanda hivyo.
Mwenyekiti wa Bodi Kampuni ya PASS, Taus Mbaga akizungumza katika wiki hiyo ya PASS amesema lengo ni kutaka kuwasaidia wakulima namna ya kuzifikia benki kwa ajili ya mikopo ,kuwakusanya wateja wapya kuifahamu PASS kwa kuachana na kuhangaika wapi watapata mikopo.

Pia alisema kupitia maonyesho hayo kampuni imelenga kutatua changamoto ya katika masuala ya kilimo,kubadilishana mawazo pamoja na kujuana.

"Tumekuwa tukifanya kazi na mabenki ili kuweza kuwasaidia wakulima wetu kupata mikopo bila mashaka na kupunguza umaskini,kuongeza Pato la Taifa ,kuweka usalama wa chakula kuweka mafunzo kwa wajasiriamali.

"Kwa sasa tuna benki 14 tunafanya nao kazi huku ajira milioni 2.5 kwa vijana zimetolewa, hivyo tunaendelea kuboresha huduma ili kuzidi kukuza uchumi katika kilimo,"amesema Mbaga.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anton Mtaka amesema kuwa, mkoa huo inatarajia mchango mkubwa kutoka Kampuni ya PASS ambapo mkoa huo unahamasisha wananchi kilimo cha zabibu, hivyo Pass iweke mchango kwa wakulima na watengeneza mchuzi.

Ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa hii ya wiki ya PASS kuja kuona shughuli za kilimo teknolojia,mazao,bidhaa na waweze kuyafanyia kazi kwenye maeneo yao huku wataalamu wakitumia nafasi hiyo kuwasaidia wananchi.

Mmoja wa wanufaika na Kampuni ya Pass wamesema, "Tunashukuru sana pass inaonyesha Ni Kiasi gani inajali wakulima wake tumepata mkopo ambao umetusaidia Katika kilimo nankuzalisha wine kuingia sokon,"amesema mmoja wa wanufaika kutoka kiwanda cha Wine Dodoma.

Nae Rhoda Joseph amesema kuwa, kupitia Kampuni ya Pass ameweza kuwasomesha watoto na kujenga nyumba ya kisasa kutokana na kilimo.

"Niwaombe watanzania wenzangu hususani wanawake wenzangu tusiache fursa hiyo kutoka PASS itatiusaidia kujikwamua Katika umaskini na kuachana kuwa tegemezi kwenye familia zetu,"amesema Rhoda .

Ikumbukwe kuwa, Jumamosi wanatarajia kuwa na uzinduzi wa Kampuni ya kilimo ambayo itazinduliwa na Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news