Albert Chalamila:Nilijiandaa kutumbuliwa ukuu wa mkoa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza,Albert Chalamila amesema kuwa hakushtuka baada ya kutenguliwa kwake kwa sababu ni jambo la kawaida katika nafasi za uteuzi.
Chalamila aliyewahi pia kuwa mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo katika mazungumzo na Ebony Fm leo.

Amesema kuwa, hajawahi kulalamikia kutenguliwa kwake kwani sababu za kutolewa kwake zimebaki katika Mamlaka ya Uteuzi

Akizungumzia mshtuko alioupata kufuatia kifo cha Rais Dkt. John Magufuli, Chalamila amesema katika maisha yake hakuwahi kuamini kuwa Rais aliyeko madarakani nchini Tanzania anaweza kufariki.

Ukomo wa utumishi wa RC Chalamila ulifikia tamati Ijumaa ya Juni 11,2021baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na kuteua wengine.

Katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alihamia Mkoa wa Mwanza ambapo aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, Albert Chalamila uteuzi wake ulitenguliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news