DC Kanali Thomas aagiza wavaa vimini,milegezo wakamatwe

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha.
Miongoni mwa mavazi hayo nii vimini na suruali za milegezo wilayani kwake.

"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Kanali Thomas wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo,

Kanali Thomas amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo wilayani humo.

Wakati huo huo amekemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Agizo hilo linafanana na la Februari 20, 2018 ambapo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya,Rehema Madusa aliliagiaza Jeshi la Polisi kuwakamata wadada wote wanaovaa nguo nusu utupu na wanaofanya biashara ya kuuza miili yao ili wakasaidie ujenzi wa nyumba za Jeshi la Polisi.

Alisema wale wote watakaomatwa adhabu yao itakuwa kufyatua tofali zitakazosaidia katika ujenzi wa nyumba za askari polisi kwa kuwa kulikuwa kuna changamoto kubwa ya makazi ya askari.

Pia maagizo hayo yanafanana na maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru baada ya kuazimia kuwachapa viboko vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya makalio pamoja na wanawake wanaovaa sketi fupi na suruali zinazobana.

Azimio hilo pia lilielekezwa kwa wanafunzi wanaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo bila sababu za msingi.

Mkutano huo ulipitisha maazimio saba yanayolenga kurejesha nidhamu na heshima kijijini Olgilai ambapo lilifikiwa kutokana na vijana wa kike na kiume kuvaa nguo zisizo na heshima.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.

“Viongozi wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo tumeambatanisha barua kwenu,”alisema Boaz na kuongeza:

“Viongozi wa dini tumewaandikia waraka huu tukijua kwamba ninyi ni watu muhimu katika kusaidia jambo hili na kuwafikishia taarifa waumini wenu wote wakubwa kwa wadogo.”

Mwenyekiti huyo alisema kwa kauli moja uongozi mkutano huo uliafiki suala hilo na kuamuru lianze kutekelezwa.

Aliyataja maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalumu watachapwa viboko.

Jingine ni kuwachapa viboko wote watakaovaa nguo zisizofaa katika jamii yao mfano sketi fupi, suruali zilizobana kwa wasichana na akina mama.

“Vijana wa kiume wanaovaa suruali zinazojulikana kama mlegezo, uendeshaji ovyo wa pikipiki, wavutaji wa bangi, dawa za kulevya, gongo na wanywaji wa viroba, uchezaji kamari na karata.

“Wanaotukana ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga shambani watashughulikiwa,” alisema Boazi.

Alisema Mkutano Mkuu wa Kijiji ulijiridhisha kuwa matendo hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa nidhamu kijijini hapo na maeneo mengine.

MUHIMU


UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news