DC Shekimweri atoa maagizo kwa DUWASA kuhusu ankara za maji

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir shekimweri ameiomba Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) mkoani hapo kuangalia kwa usahihi kiwango cha bei ya Ankara za maji kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kubambikiwa bei kubwa tofauti na matumizi yao
Shekimweri ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akifungua semina ya madiwani wa jiji hilo iliyoandaliwa na DUWASA kwa lengo la kutoa elimu kuhusu majukumu na wajibu wa madiwani kuelewa kazi zinzofanywa na DUWASA.

Amesema, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kulipa bei kubwa ya Ankara za mji, hivyo ni muhimu kutambua chanzo cha tatizo ambalo huenda likasababishwa na usomwaji vibaya wa mita za maji au uharibifu wa miundombinu.

Aidha,Shekimweri ameiomba mamlaka hiyo kudhibiti upotevu wa maji, uaharibifu wa miundombinu ya maji pamoja na wizi wa miundombinu ya maji ikiwemo mabomba ili kudhibiti upotevu wa maji wa asilimia 30 uliopo kwa sasa.
Meya wa jiji hilo, Profesa Denis Mwamfupe alisema, madiwani wana nafasi kubwa ya kushiriki katika masuala ya maji kwa kuwa wao wanawakilisha kundi kubwa la watu, hivyo kupata semina hiyo kutawawezesha Duwasa kufanya kazi kwa ufanisi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph alimuhakikishia Mkuu wa Wilaya kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa kwa kuhakikiasha wanadhibiti upotevu wa maji pamoja na kufuatilia kiwango cha bei za maji.

Wakizungumza kwenye semina hiyo baadhi ya madiwani waliishukuru DUWASA kwa kupatiwa semina hiyo na kuomba mamlaka hiyo kuhakikisha wanafikisha maji katika maeneo ambayo tayari wameshayawekea miundombinu.

Mbali na hayo madiwani hao wameongeza kuwa kutokana na maeneo mengi kuonekana kuwa na changamoto ya maji waliiomba mamlaka hiyo kufika kwa wakati wanapopata taarifa ya uharibifu wa miundombinu kwenye maeneo ambayo kumetokea uharibifu huo.

Walisema kuwa, kufika kwao kwa wakati kutapunguza kero zinazojitokeza baada ya miundombinu hiyo kuharibika ikiwemo kukosa maji kwa baadhi ya maeneo.MUHIMU

UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Post a Comment

0 Comments