DC Siriel:Wanaume acheni kunyonya maziwa ya wake zenu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wanawake wanaonyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga, wamemuomba Mkuu wa wilaya hiyo, Siriel Mchembe kuwasaidia kupaza sauti na kukemea wanaume wao kuacha tabia ya kuwanyonya maziwa.

Ni kwa sababu wanawafanya watoto wasipate maziwa ya kutosha.

Rai hiyo wameitoa Agosti 10, 2021 kwa Mchembe kwenye maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika mji mdogo wa Mkata.

Amesema kuwa, ana taarifa kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa na tabia hiyo wakihusishwa na imani za kishirikina.

"Niwashauri wale wanaume mnaonyonya maziwa ya wake zenu muache, mnatumia chakula cha watoto wenu na hiyo inasababisha mtoto kupata utapiamlo maana hapati maziwa ya kutosha, la msingi hakikisheni mnashirikiana kwenye malezi haya mambo mengine acheni,"amesema DC Mchembe.

Aidha,Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Julia Charo amesema kuwa hadi Juni 21, mwaka huu watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano waliobainika kuwa na uzito pungufu ni watoto 3,856 sawa na asilimia 14 ya watoto wote waliohudhuria kliniki.

Amesema,kwa upande wa watoto waliopata udumavu ni asimilia 34 ya watoto wote waliopelekwa na kuhudumiwa katika kliniki na wajawazito 7519 waliopimwa wingi wa damu 102 walikutwa na upungufu mkali wa damu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news