EWURA yafungia vituo 26 vya mafuta

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imevifungia vituo 26 vya mafuta na kuvitoza faini kwa kosa la kukwepa kodi na kukutwa na mafuta yasiyokidhi viwango.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje ameyasema hayo katika mazungumzo na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam.

Amesema, zoezi la ukaguzi lilianza Julai 2, mwaka huu na lilifanyika katika mikoa ya Kanda ya Mashariki,Kanda ya Ziwa,Kanda za Juu Kusini,Kanda ya Kati ambapo hadi kufikia Agosti 9, mwaka huu

Kiongozi huyo amesema, katika ukaguzi huo jumla ya vituo 195 vilikaguliwa ambapo vituo 26 sawa na asilimia 13.33 vilikutwa na mafuta ambayo hayana kiwango stahiki cha vinasaba ikiwemo Lake Oil Company cha Geita,GBP Oil cha Mwanza, Total Tanzania Mwanza,Azhad Abdulrahim Mkuranga,Ally Adon ya Mombasa.

“Kwa mujibu wa kanuni kampuni zenye 'depots' zinatakiwa kuhakikisha mafuta yote yaliyonunuliwa kwa ajili ya soko la ndani yanawekewa vinasaba na mfanyabiashara yeyote anayenunua mafuta anatakiwa kuhakikisha yanawekwa vinasaba kwa usahihi kwenye gari likilobeba mafuta,"amesema Chibulunje.

Amesema, baada ya TBS kukabidhi EWURA mashine za kung’amua vinasaba kwenye mafuta walianza zoezi la ukaguzi kwenye vituo vya mafuta ili kuhakiki kama mafuta kwenye vituo hivyo yana kiwango sahihi cha vinasaba na kubaini changamoto hiyo.

"Hii ina maanisha kuwa wamiliki wa vituo hivyo walichanganya mafuta yao na mafuta ambayo hayajalipiwa kodi wakitaka kukwepa kulipa kodi stahiki. Ewura imevifungia vituo vyote vilivyohusika na kuvilipisha faini kwa mujibu wa kanuni na tayari taarifa zao zimepelekwa TRA," amesema.

Chibulunje amesema ka mujibu wa kanuni vituo hivyo vimetozwa faini ya Sh7 milioni na Ewura kwa kosa hilo lakini pia TRA wamekabidhiwa taarifa zao ili waweze kufanya tathimini ya kodi iliyokwepwa, na kituo kitafunguliwa baada ya kulipa faini na kodi inayodaiwa na TRA.

Kaimu Mkurugenzi huyo amewaasa wafanyabiashara wote kufanya biashara zao kwa kufuata taratibu za sheria zilizowekwa ili kuepuka usumbufu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news