Hakainde Hichilema baada ya vipindi vitano kuambulia patupu,ndoto yake imetiki ya urais

NA MWANDISHI DIRAMAKINI, Lusaka

Tume ya uchaguzi wa Zambia imemtangaza kiongozi wa upinzani, Hakainde Hichilema kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais.

Ushindi huo unakuja kutokana na uchaguzi wa Alhamisi iliyopita ambao ulijaa heka heka za hapa na pale huku baadhi ya wapinzani wakidai kunyanyaswa.

Hakainde Hichilema ambaye ni mfanyabiashara na mwanasiasa wa Zambia anakuwa Rais mteule baada ya kuisaka nafasi hiyo kwa vipindi vitano bila mafanikio.


Rais huyo mteule mwaka 2006, 2008, 2011, 2015 na 2016 aligombea na kuambulia patupu, lakini ndoto yake imekuwa kweli uchaguzi wa 2021.

Aidha, licha ya kitisho cha Rais aliyekuwepo Edgar Lungu cha kutishia kuyakataa matokeo, wafuasi wa Hakainde Hichilema ambaye ni mbobezi katika masuala ya uchumi wamesema, hoja ya Lungu haina mashiko

Waliyathibitisha hayo kabla na baada ya matokeo rasmi kutangazwa ambapo wafuasi wa Hakainde Hichilema na chama chake cha United Party for National Development, UPND walimiminika katika mitaa ya mji mkuu Lusaka na kushangilia

Mbele ya waandishi wa habari na wadau wengine, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zambia, Esau Chilu amesema, baada ya matokeo kutoka majimbo 155 kati ya 156 anamtangaza Hichilema kuwa mshindi.

''Hichilema, Hakainde, S; kura 2,810,777 na Mheshimiwa Lungu kura 1,814,201. Kwa hiyo namtangaza Hichilema Hakainde S, kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Zambia, leo Agosti 16,mwaka 2021,'' amesema Chilu.

Baada ya kutangazwa mshindi, Hichilema ambaye ni mfanyabiashara tajiri aliweka picha yake katika mtandao wa Twitter akiwa mbele ya wafuasi wake, na kuweka ujumbe akisema, ''Asante Zambia''.

Rais Lungu amekuwa madarakani kwa miaka sita na alijaribu kila awezelano kupata muhula mwingine, licha ya kupoteza umaarufu kutokana na kudorora kwa hali ya maisha na kukosolewa kuukandamiza upinzani nchini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news