Mbunge awapa pole wafiwa wa Kijana aliyeuawa na kufukiwa shimoni Mbagala

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Mheshimiwa Abdallah Chaurembo leo Agosti 2, 2021, amewatembelea na kuwapa pole wafiwa kufuatia msiba wa kijana Shabani Amir Mbalali (20) aliyeuawa na kufukiwa shimoni siku ya Ijumaa ya Julai 30,2021.

Tukio hilo lilitokea katika msitu wa UVIKIUTA uliopo Chamazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza katika msiba huo Mheshimiwa Chaurembo aliwataka wafiwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Sambamba na kuitaka serikali kuikata Wilaya ya Temeke na kupata Wilaya mpya ya Mbagala ili kupunguza matukio ya kihalifu yanayozidi kutokea kila siku kwa sababu ya umbali wa huduma za kipolisi unaosababishwa na ukubwa wa Wilaya ya Temeke hususani Jimbo la Mbagala.
"Niliposikia tukio hili nilisikitika sana, yaani imefikia hatua watu wanamuua binadamu mwenzao kwa sababu ya mbuzi watano," amesema Chaurembo.

"Nichukue nafasi hii kuwapa pole wafiwa, tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu, Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amen," amesema Chaurembo.

"Sambamba na hilo jimbo letu limekuwa kubwa hii inatokana na kuwa na wilaya moja tu ya Temeke, naomba serikali iikate Wilaya ya Temeke na kupata wilaya nyingine ya Mbagala, kwa sababu viongozi wa kipolisi wataweza kufika mpaka pembezoni mwa jimbo letu na hatimaye kuweza kudhibiti matukio haya ya kihalifu,"amesema Chaurembo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news