Mbunge mstaafu na msanii Profesa Jay asajiliwa rasmi kuwa Mtangazaji Clouds FM

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Msanii wa muziki, Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa Jay ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi kati ya 2015 hadi 2020 amesajiliwa rasmi kuwa Mtangazaji Clouds FM.

"Jana kwenye mitandao yetu ya kijamii tulisema leo kwenye PowerBreakFast kwa mara ya kwanza utasikia sauti ya usajili mpya. Ladies and gentlemen na huyu ni ProfessorJayTz ndiyo usajili mpya ndani ya PB,"wameeleza Clouds Media.
Msanii huyo wa muziki wa Rap alitangazwa mshindi katika Jimbo la Mikumi katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 32,259.
Profesa Jay kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA alimshinda mpinzani wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jonas Nkya ambaye alijipatika kura 30,425 ingawa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hakuweza kutetea nafasi yake.

MUHIMU

UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news