Mbunge Mwanafa apata ajali akielekea bungeni usiku huu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mbunge wa Muheza, Hamis Mwijuma maarufu kama Mwana FA amepata ajali katika eneo la Mkambarani mkoani Morogoro.

Ni baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na gari ndogo aina ya Toyota Crown iliyokuwa ikijaribu kulipita gari lake wakati akitoka Dar es Salaam kuelekea jijini Dodoma.
Katika ajali hiyo, watu wawili ambao walikuwa ni abiria kwenye gari aina ya crown wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mororgoro, Fortunatus Musilim amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli Mheshimiwa Mbunge amepata ajali, ila yuko salama. Amepata ajali majira ya saa mbili usiku baada ya gari aina ya Toyota Crown iliyokuwa na abiria wanne kujaribu kuipita gari yake,” amesema Musilim.

“Hata hivyo Mheshimiwa Mbunge alitumia gari lake kuwapeleka majeruhi katika hospitali ya Mkoa,”amesema.

Kamanda Musilim amesema, watu wengine wawili waliokuwa kwenye Crown walipata michubuko kadhaa na wako salama.

Mheshimiwa Mwanafa amesema kuwa, "Tulikuwa wawili mimi na dereva wangu tulitoka Muheza tukapita Msoga Rais Mstaafu alikuwa amefiwa na mtoto wa kaka yake, tukawa tunatoka tunaelekea Dodoma hii sehemu inaitwa Kingolwira kuna malori mengi yanaelekea Dar, kuna mtu akawa ana overtake.

"Namshukuru Mungu tumetoka salama, mimi nina maumivu kidogo kifuani na kwenye mkono wa kushoto, lakini napata huduma hapa kwenye hospitali ya mkoa hapa Morogoro,"amesema Hamis Mwinjuma ambaye ni Mbunge wa Muheza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news