Mtanzania Mwinjilisti Temba aiongoza Botswana katika maombi dhidi ya Corona

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Baada ya Serikali ya Jamhuri ya Botswana kutumia kila mbinu ikiwemo chanjo ya UVIKO-19 huku matokeo yakiwa hayaridhishi, hatimaye wameitikia wito wa maombi ya Kitaifa kutoka kwa Mwinjilisti wa Kimataifa na Mtanzania, Alphonce Temba.
Ni muda mfupi baada ya Mwinjilisti Temba kufika Ikulu na kukutana na Waziri anayehusika na Masuala ya Rais, Utumishi na Utawala wa Umma, Mheshimiwa Kabo Neale Sechele Morwaeng.

Temba ambaye ni Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam alipokelewa mjini Gaborone, Botswana akitokea nchini Zambia.

Alikuwa Zambia ambapo awali alipokelewa kwa shangwe baada ya utabiri wake kuhusu ushindi wa Chama cha Upinzani cha United Party for National Development (UPND) kushinda urais kutimia.

Akizungumza baada ya kuwasili Botswana, Mwinjilisti Temba amesema, ameendelea kuitikia wito wa Mungu wa kwenda kutamka neno la uponyaji na ushindi kwa mataifa mbalimbali Kusini mwa Afrika.

Maombi yanaweza kuwa silaa tosha. Ikizingatiwa kuwa, Botswana walifungia watu ndani na kila wiki waligawa chakula nyumba zote nchi nzima na nusu ya wananchi wamechanjwa, lakini imekuwa na vifo vingi ikifuatiwa na India kwa sasa kulingana na takwimu za mara kwa mara.

"Ninamshukuru Mungu, baada ya kuingia Ikulu na kupokelewa na Waziri Ofisi ya Rais, Mheshimiwa Kabo baada ya maongezi pamoja na washauri wa rais wakakubaliana nami kuwa sasa Botswana kwa mara ya kwanza Serikali iitishe maombi ya mwezi mzima kumlilia Mungu.

"Kusudi Mungu aponye nchi na vizuizi viachilie. Jambo hilo limeleta mjadala sana kutoka baadhi ya madhehebu hapa kuwa, kwa nini mtumishi mgeni toka Tanzania atumike kuanzisha maombi, lakini Bwana akaingilia kati na maombi yanaendelea.

"Nawashukuru watanzania kwa maombi yenu, lakini kilichoniletea heshima zaidi ni kwa sababu ya Hayati Rais Dkt.John Pombe Magufuli,kwani wakati korona ilipoingia nchini, mara ya kwanza na kuwatangazia watanzania na Dunia kuwa Mungu atatuondolea korona mmoja wa mbunge wa Botswana katika Bunge aliomba Bunge kutoa kauli ya maombi, lakini Makamu wa Rais hapa akaipinga na kudai wako kwenye jambo zito na maombi hayana nafasi katika hilo.

"Ndipo hali ikazidi kuwa mbaya zaidi kila leo mpaka Mungu alivyonileta kuitisha maombi ya Kitaifa,Mungu apewe sifa na utukufu, na mataifa na wenye mamlaka kudharau maombi katika mataifa yao mwisho ni aibu na fedheha,"amesema Mwinjilisti Temba.

Baadae Mwinjilisti Temba alielekea katika Kanisa la Holy Ghost Church House Int lililopo mjini Gaborone, Botswana ambalo linaongozwa na Mchungaji Apostle Jackson Kgopolo tazama video chini;Post a Comment

0 Comments