Milioni 400/- kupelekwa Kituo cha Afya Kamanga Feri wilayani Sengerema

Na Nteghenjwa Hosseah, Sengerama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema Serikali itapeleka Shilingi Mil 400 kwenye Kituo cha Afya Kamanga Feri Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerem Mkoani Mwanza.
Amesema, fedha hizo ni kwa ajili ya kutatua changamoto iliyokuwepo katika Kituo hicho na kupitia fedha hizo Kutajengwa Chumba cha Upasuaji pamoja na Wodi ya Mama na Mtoto.

Akiwa ziarani Wilayani humo mapema leo Tar 14.08.2021 Mhe Ummy alijulishwa changamoto ya kituo hicho kuwa ni kukosekana kwa chumba cha upasuaji, upungufu wa watumishi pamoja na mafuriko pale Ziwa Victoria linapofurika.
Aliweka wazi kuwa Watumishi wanaojitolea watapewa kipaumbele katika ajira zijazo na kuhusu Mafuriko kutoka Ziwani aliwashauri Uongozi wa Wilaya kuwasilisha andiko Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambapo watapata suluhisho kutokana na changamoto hiyo inayosababishwa na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.

Kituo cha Afya Kamanga kinahudunia Wakazi Takribani elf 60 wa Kata za Kamanga, Katunguru, Ngoma B na Kahunulo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news