Mkutano Mkuu wa Uchaguzi TFF kufanyika kesho Tanga, wageni kutoka CAF, FIFA kushuhudia

NA OSCAR ASSENGA,TANGA

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau amesema mkutano mkuu wa Kawaida wa Shirikisho ambapo moja ya ajenda kubwa ni Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika jijini Tanga kesho.

Ambapo maandalizi yake yamekamilika kwa asilimia 95 kwa wageni mbalimbali wakiwemo wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wakitarajiwa kuhudhuria mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuelekea mkutano huo.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach jijini hapa huku asilimia tano ya wajumbe iliyobakia ikitarajiwa kuwasili leo kuungana na wenzao kwa ajili ushiriki wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Tanga Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), Wilfred Kidau alisema kwamba maandalizi yamekamilia huku wageni mbalimbali wakiwasili ikiwemo Rais wa Shirikisho la Soka nchini Somalia ambaye pia vilevile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
Mgombea Urais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari leo

Amesema, pia walikuwa na kamati ya uchaguzi wa TFF kuhakikisha maandalizi muhimu yanakamilika na wao kama sekretarieti ni wajibu wao kuhakikisha kamati ya uchaguzi ili iweze kufanya mambo yake kwa asilimia 100.

Amesema, wapo wageni wengine mbalimbali wameanza kuwasili jijini Tanga ambapo wegine wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) wakiwemo wajumbe wawili wawili wapo njiani tayari kutua jijini Tanga.

Awali akizungumza na waandishi wa Habari Mgombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia alisema kikatiba kila baada ya miaka minne wanafanya uchaguzi na mwisho ulifanyika mwaka 2017 na safari hii wanafanya AgostI 7 na wanafanya uchaguzi huo hapa jijini Tanga huku akiwaomba watanzania wawaombee kwa ajili ya mkutano huo.
Amesema kwamba,mkutano huo utajadili taarifa zao za utekelezaji za mwaka na yeye atatoa taarifa yake ya miaka minne ya uongozi wake na wajumbe watajadili na baada ya hapo wataenda kwenye uchaguzi huo.

Pia amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwenye mkutano huo, mgombea wa
Urais atakuwa pekee yake na uthibitisho utafanyika kwenye mkutano huo, hivyo
anaomba wajumbe waweze kumthibitisha.

Naye Mwenyekiti wa timu ya Biashara United ya Mara, Selemani Mataso alisema uchaguzi huo ni muhimu sana hasa wao viongozi wa vilabu wanahitaji kupata watu ambao watawasaidia kuhakikisha wanaenda
kutengeneza muonekano wa mpira, ambayo haiwezi kuwa na shida na kuweka usawa wa
vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news