Baraza la Ushindani (FCT limeendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kutumia teknolojia za kidijitali, likiwataka wananchi na wadau kutumia mfumo wa kielektroniki kuwasilisha mashauri na rufaa zao kwa urahisi na kwa wakati.










Msajili wa Baraza la Ushindani, Mbegu Kaskasi, amesema Baraza hilo lililo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara lina jukumu la kusikiliza na kutatua migogoro ya ushindani wa biashara na udhibiti wa soko inayotokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na mamlaka za udhibiti zikiwemo TCRA, EWURA, LATRA, TURA na TCAA.Kaskasi amesema Baraza hilo linaundwa na Jaji wa Mahakama Kuu pamoja na wajumbe sita, huku likitumia fursa mbalimbali kuwaelimisha wananchi kuhusu majukumu yake, namna ya kupata huduma na utaratibu wa kuwasilisha mashauri, ikiwemo kupitia mfumo wa kielektroniki wa usikilizaji wa mashauri.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















