MWAUWASA na kasi ya kipekee katika kuwahudumia wananchi maji safi na salama

HISTORIA FUPI YA MWAUWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (MWAUWASA) ilianzishwa Julai 1, 1996 kwa uamuzi uliofanywa na Wizara ya Maji kuanzisha Mamlaka za maji chini ya Bodi ya Ushauri katika hali ya kugharimia sehemu ya uendeshaji (semi-autonomous). 

Uamuzi huo ulihalalishwa na sheria ya maji kwa wakati ule, sheria namba 8 ya mwaka 1997. Serikali iliipandisha MWAUWASA kuwa Daraja ‘A’ ili kujiendesha bila kupata ruzuku yoyote kutoka serikalini (full autonomous) kwa Waraka wa Serikali namba 61 wa tarehe 13/02/1998.
Umiliki na Majukumu ya MWAUWASA

MWAUWASA inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100. 

Ikiongozwa na DHIMA na ADHIMA yake, MWAUWASA inatekeleza majukumu yake ya kutoa huduma ya majisafi na uondoshaji majitaka (usafi wa mazingira) Jijini Mwanza katika wilaya za Nyamagana na Ilemela pamoja na eneo la Kisesa wilayani Magu. 

Majukumu hayo yanatekelezwa kwa kuzingatia Sheria ya Majisafi na Usafi wa Mazingira namba 12 ya mwaka 2009; Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002, Miongozo mbalimbali toka EWURA; Mkataba wa Utendaji (performance contract) kati ya Wizara ya Maji na MWAUWASA pamoja na miongozo mingine mbalimbali inayotolewa mara kwa mara na Wizara ya Maji. Endelea hapa>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news