Oman yaondoa katazo kwa abiria kutoka Tanzania kuingia nchini humo

NA MWANDISHI MAALUM

Ubalozi wa Oman unapenda kuwajulisha kuwa Serikali ya Oman imeondoa katazo la kuingia Oman kwa abiria kutoka Tanzania na nchi zingine zilizokuwa kwenye kundi hili.
Hivyo basi kuanzia tarehe 1 Septemba 2021 abiria wanaopandia ndege zao Tanzania kuja Oman wataruhusiwa kuingia Oman kwa kutimiza masharti yafuatayo:

1. Kuwa na cheti cha chanjo ya Uviko- 19 (COVID-19) kinachothibitisha kuwa abiria
amekamilisha dozi mbili za chanjo au dozi moja ya chanjo kwa zile ambazo dozi ni moja chanjo iwe imefanyika sio chini ya siku 14 kabla ya tarehe ya kuingia Oman

2. Cheti cha chanjo ni lazima kiwe na alama ya QR (QR Code)

3. Chanjo iliyotumika ni lazima iwe miongoni mwa chanjo zilizoidhinishwa kutumika nchini
Oman

4. Chanjo zilizoidhinishwa Oman ni Johnson and Johnson, AstraZeneca-Oxford, AstraZeneca-Covishield, Pfizer ,Sinopharm, Sirovac, Sputnik na Moderna

5. Cheti cha kupima Uviko- 19 kinachoonyesha kutokuwa na maambukizi (Negative PCR Test Certificate ), vipimo vifanyike saa 72 kabla ya safari

Pamoja na kuwa suala la chanjo linabaki kuwa hiari ya mtu binafsi, lakini ni muhimu kufahamu kuwa hiari hii inakoma pale tu masharti, maelekezo na ya umma (public health) katika nchi mnayoishi zinapoelekeza vinginevyo au masharti ya mwajiri wako yanapoelekeza vinginevyo kwa hali hii mnatakiwa kuzingatia kuwa serikali ya Oman imetoa maelekezo kuwa kuanzia tarehe 1 Septemba 2021 wale wote wanaoingia kwenye maeneo ya umma na yenye mikusanyiko ya watu (PUBLIC PLACES) kama vile maofisi, maduka makubwa, hospital, usafiri wa umma na viwanja vya ndege ni lazima wawe na vyeti vya kuonyesha wamepata na kukamilisha chanjo ya UVIKO-19.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news