Picha: Mkutano wa Chama cha Waendesha Mashtaka Afrika Mashariki unaoendelea jijini Arusha


Rais wa Chama cha Waendesha Mashtaka Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Tanzania(DPP), Mheshimiwa Sylvester Mwakitalu akiongoza kongamano linalohusiana na masuala mbalimbali yahusuyo wanyamapori na ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na uhalifu.Kongamano hilo linafanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya,DPP Noordin Haji akiendelea kufuatilia Mkutano Mkuu wa tisa wa mwaka wa chama hicho, unaofanyika jijini Arusha leo Agosti 30 ikiwa ni siku yake ya kwanza ya mkutano huo.
Julie Thomson ambaye ni Mkurugenzi wa Mradi wa kupambana na Usafirishaji haramu wa Wanyama, Ukanda wa Afrika Mashariki akiwa sehemu ya wazungumzaji katika Mkutano Mkuu wa tisa wa mwaka wa Chama cha Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha leo Agosti 30 ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano huo.
Rais wa Chama cha Waendesha Mashtaka Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania, Mheshimiwa Sylvester Mwakitalu akizungumza katika mkutano mkuu wa tisa wa mwaka wa Chama hicho,cha Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa tisa. (Picha zote na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Tanzania)




Chama cha Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na jumla ya wanachama wa nchi tano zikiwapo Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na Kenya. Hadi kufikia hivi sasa chama hicho kimefanikiwa kuongeza wanachama kutoka nchi nyingine jirani zikiwemo Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Sudan, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbiji

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news