Rais Dkt.Mwinyi ateta na Mabalozi wa Ujerumani, Rwanda na Kuwait

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 25, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe.Mubarak Mohammed Alsehaijan, alipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Kasha mgeni wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe.Mubarak Mohammed Alsehaijan, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Mubarak Mohammed Alsehaijan, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
 
Awali Rais Dkt,Mwinyi alikutana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mubarak Mohammed Alsehaijan.

Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuendeleza uhusiano wa kihistoria kati yake na Zanzibar pamoja na kuipatia Zanzibar misaada mbalimbali katika sekta za kijamii.

Katika hatua nyingine,Rais Dkt. Mwinyi alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda, Meja Jenerali Charles Karamba.
Katika mazungumzo hayo Balozi Karamba alimueleza Rais mpango wa Shirika la Ndege la Rwanda ‘Air Rwanda’ kuanza safari zake kati ya Kigali na Zanzibar ifikiapo katikati ya mwaka 2022, hatua ambayo itaimarisha sekta ya utalii kwa Zanzibar na Rwanda.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Mhe.Maj.Gen.Charles Karamba, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, leo 25/8/2021.(Picha na Ikulu) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe.Regina Hess, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazunguzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo na Ushirikiano Ubalozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Dr.Katrin Bornemann, wakati wa mazungumzo na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe. Regina Hess.(kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Balozi Karamba alitumia nafasi hiyo pia kumtaarifu Rais juu ya mwaliko maalum waliouleta Zanzibar wa kuanzisha Ushirikiano baina ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB) unaolenga ushirikiano wa kiuwekezaji na kuwa na kituo kimoja cha kibiashara baina ya Zanzibar na Rwanda.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regina Hess ambaye alifika Ikulu Zanzibar kuelezea mipango ya ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Zanzibar na Ujerumani hususani kwenye eneo la uboreshaji wa huduma za maji na michezo.

Mapema hii leo,Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alikutana na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika Jamhuri ya Slovakia Bwana Moustafa Khataw ambaye alimtaarifu Mhe. Rais mpango wa kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Slovakia mpaka Zanzibar.

Kwa upande wake Rais Dkt. Mwinyi alimtaka mwakilishi huyo kushajiisha wawekezaji wa Slovakia na kusisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatilia mkazo dira ya Uchumi wa Buluu, ikiwemo uvuvi wa bahari kuu pamoja na Mafuta na Gesi huku akibainisha kuwepo rasilimali za kutosha baharini ambazo bado hazijatumika ipasavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news