Mkulima aliyetaka kuzila sehemu za siri, maini ya mtoto akamatwa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Harold Hhando ambaye ni mkulima wa Mtaa wa Silaloda Mji wa Mbulu mkoani Manyara anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kaka yake Emmanuela Hhando (13) na kumtoa viungo vya mwili.
Mkulima Hhando anadaiwa alimuua mtoto huyo wa kaka yake kwa kumpasua katikati ya miguuu na kumtenganisha vipande viwili kisha kukata sehemu za siri, kumtoa maini na kutaka kuyapika ili ayale.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marrison Mwakyoma, amesema, tukio hilo lilitokea kijijini hapo.

Kamanda Mwakyoma amesema, chanzo cha tukio hilo ni ushirikina kwani Hhando ameeleza kuwa aliambiwa na mungu wake amuue mtoto wa kaka yake na kula maini ili avune mazao mengi.

Alisema, Hhando ni mkulima wa eneo hilo la Silaloda hivyo imani za kishirikina zimesababisha akamuua mtoto huyo kwa kumpasua na kudai kuwa ameoteshwa kufanya hivyo.

“Mtuhumiwa anadai kuwa ameoteshwa na mungu wake na ana akili zake timamu hivyo alitarajia kula viungo hivyo ili aweze kupata mazao mengi zaidi shambani kwake,” amesema Kamanda Mwakyoma.

Ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutojihusisha na imani za kishirikina na kusababisha mauaji kama hayo ya kikatili ikiwemo kuuawa ndugu kwa ndugu.

Naye mkazi wa mtaa wa Silaloda, Johna Baynet alisema wananchi wa eneo hilo wamesikitshwa na kitendo hicho cha Hhando kumuua binti huyo mdogo ambaye ni mtoto wa kaka yake.

“Hhando hakuwa na matukio mabaya ila tumeshangazwa na mauaji hayo ya kikatili aliyomfanyia mtoto wa kaka yake kwani hana taarifa za matukio ya uhalifu,” amesema.

MUHIMU

UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news