Rais Samia ampongeza Rais mteule wa Zambia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Saa chache baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Zambia kumtangaza Hakainde Hichilema wa Chama Cha United Party for National Development (UPND) kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa kupata kura 2,810,777, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempongeza.

Hichilema amemshinda, Edgar Lungu, Rais anayemaliza muda wake kutoka katika Chama cha Patriotic Front (PF) aliyejinyakulia kura 1,814,201.Zinazohusiana;Ndoto yake imetiki
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Zambia, Esau Chulu leo Jumatatu tarehe 16 Agosti 2021 ndiye aliyetangaza matokeo hayo.

Kinyang’anyiro cha Urais nchini Zambia, kiliwashirikisha wagombea 16 katika uchaguzi mkuu uliofanyika, Jumapili tarehe 8 Agosti 2021.

Wananchi milioni saba nchini Zambia walikuwa wamejiandikisha kupiga kura kati ya wakaazi milioni 19.

Kupitia ukuta wake wa Twitter, Rais Samia amempongeza Hakainde Hichilema kwa ushindi huo.
"Kwa niaba ya Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali, nakupongeza Mhe.Hakainde Hichilema kwa ushindi ulioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia. Ushindi huo ni uthibitisho wa imani ya wananchi wa Zambia kwako. Naahidi kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu,"ameeleza Rais Samia.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameieleza DIRAMAKINI Blog kuwa, matokeo haya ni ushawishi mkubwa wa vijana nchini Zambia ambao wanataka kuona mageuzi makubwa katika uchumi wa Zambia.

Sambamba na fursa za ajira hasa miongoni mwa vijana wa kizazi kipya nchini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news