RC Tabora aagiza usimamizi mzuri miradi ya maendeleo

NA TIGANYA VINCENT

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt.Batilda Buriani ameziagiza Halmashauri za Wilaya kuhakikisha zinasimamia matumizi sahihi ya fedha zinazopewa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuleta matokeo mazuri kwa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi, Dkt.Batilda Buriani akitoa hotuba leo ya uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Igunga.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Igunga.

Ametoa kauli hiyo leo mjini Igunga wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya.

Balozi Dkt.Batilda amesema ni lazima miradi ya maendeleo inayojengwa katika maeneo mbalimbali ya wananchi ilingane na thamani halisi ya fedha inayotolewa na Serikali.

“Hakikisheni mnasimamia vema utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili ijengwe kwa viwango vilivyokusudiwa na msisite kuchukua hatua kali kwa watendaji ambao watatekeleza miradi chini ya kiwango,” amesisitiza.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo akifungua kikao cha uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya yake.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Igunga wakiwa katika uzinduzi wa Baraza leo. (Picha na Tiganya Vincent).

Ameongeza kuwa, sanjari na hilo ni vema Halmashauri zikahakikisha zinaongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ikiwemo kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitawapatia fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Balozi Dkt. Batilda amesema, ukusanyaji wa mapato ni vema ukatumia njia shirikishi na Rafiki kwa wananchi balada ya kusubiri kutoza faini. “Ukusanyaji wa mapato uwe wa kirafiki zaidi badala ya kugeuza faini kama sehemu ya kukusanya mapato,” amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news