TASAF yaanza ujenzi wa Ukumbi katika Shehia ya Kizimkazi kuwezesha wanafunzi kufanya mitihani

Na James K. Mwanamyoto-Kizimkazi

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeanza ujenzi wa ukumbi utakaogharimu shilingi milioni 149 katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani, Zanzibar ili kutatua changamoto ya kukosekana kwa darasa la kufanyia mitihani kwa wanafunzi wa eneo hilo, ambapo ukumbi huo pia utatumika kwa shughuli za kijamii kwa wananchi wa shehia hiyo iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza kuhusu mradi wa ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii mara baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mradi huo unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akikagua mradi wa ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa ukumbi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema dhamira ya ofisi yake kutumia fedha za ruzuku zinazotolewa na TASAF ni kuwasaidia wanafunzi wa eneo la Kizimkazi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihangaika kutafuta maeneo ya kufanyia mitihani.

“Mradi huu utawasaidia wanafunzi ambao wakati wa kipindi cha mitihani wamekuwa wakitafutiwa maeneo mengine ya kufanyia mitihani kutokana na kukosa darasa ya kufanyia mitihani na utawasaidia pia wakazi wa Kizimkazi kupata ukumbi wa mikutano kwani ni muda mrefu wamekabiliana na changamoto hiyo,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.

Ameongeza kuwa, ofisi yake kupitia TASAF imekuwa na utamaduni wa kutoa mchango kwenye jamii kwa kutoa fedha zinazotumika kuboresha huduma kwenye sekta ya elimu, afya na miundombinu kwa lengo la kuwa karibu na jamii, kushiriki utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na hatimaye wafurahie mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akipokea maelezo ya ujenzi wa mradi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Baadhi ya wananchi Shehia ya Kizimkazi Dimbani wakishiriki ujenzi wa mradi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amesema kuwa, mradi huo wa ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii ulikuwa ni hitaji la wananchi wa Shehia ya Kizimkazi, hivyo TASAF ikaamua kufadhili ili kukidhi mahitaji ya wananchi hao.

“Ujenzi wa mradi huu unahusisha wananchi kufanya kazi za ajira ya muda ambapo kaya za walengwa 107 wa TASAF zinafanya kazi kwenye mradi huo,” Bw. Mwamanga amefafanua.
Muonekano wa mradi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa maelekezo ya ujenzi wa mradi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Bw. Mwamanga amesema, mradi huo umehusisha ushiriki wa wananchi ili waweze kutoa mchango kwenye eneo la ujenzi na kupata ujira, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kujiona ni sehemu ya mradi kwa kuchangia nguvu kazi yao.

Dhamira kuu ya ujenzi wa ukumbi huo ni kuunga mkono azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo kwa wananchi wote ikiwemo wa Shehia ya Kizimkazi ambako ndiko alikozaliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news