SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeteketeza tani 39 za bidhaa za chakula zisizokidhi matakwa ya viwango, zenye thamani ya takribani Sh milioni 149, ikiwa ni hatua ya kuwalinda wananchi dhidi ya matumizi ya bidhaa zisizo salama.
Zoezi hilo limefanyika Agosti 17, 2026, katika eneo la Mbezi Gongoni, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, baada ya bidhaa hizo kubainika kuwa na mapungufu mbalimbali wakati wa ukaguzi wa mara kwa mara uliofanywa na TBS kati ya Julai na Agosti mwaka huu.Meneja wa TBS Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bi. Noor Meghji, amesema ukaguzi huo umebaini baadhi ya bidhaa za chakula zikikosa alama ya ubora pamoja na taarifa muhimu kwenye vifungashio, hali inayoweza kuhatarisha afya za watumiaji.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















