UJENZI WA KITUO CHA HUDUMA YA PAMOJA MPAKANI (OSBP) WAFIKIA ASILIMA 67

Na Deniza Cyprian-WUU

Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa kituo cha huduma ya pamoja mpakani (OSBP) mpakani mwa Tanzania na Malawi eneo la Kasumulu unaojengwa na mkandarasi China Geo Engineering Corporation umefikia asilimia 67.1 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2021.
Mhandisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Huduma ya Pamoja Mpakani (OSBP) katika eneo la Kasumulu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Daniel Mandari, akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, mkoani Mbeya.Hayo yamesemwa mkoani Mbeya na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo hicho unaojengwa kwa awamu tatu na unagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 26.

“Nitoe wito kwa mhandisi mshauri kuusimiamia mradi huu kikamilifu ili ukamililike kama ulivyopangwa kulingana na mkataba”, amesisitiza Naibu Waziri huyo.

Aidha, Naibu Waziri Kasekenya amesema kuwa mpaka sasa mkandarasi hana madai yoyote anayodai yatakayokwamisha utekelezaji wa mradi huo.
Muonekano wa mchoro wa Kituo cha Huduma ya Pamoja Mpakani (OSBP) mpakani mwa Tanzania na Malawi katika eneo la Kasumulu utakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri wa Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Daniel Mandari, amemueleza Naibu Waziri kuwa licha changamoto zilizoukabili mradi huo kuchelewa kukamilika, mkandarasi amekwisha kamilisha ofisi za wahandisi na maabara asilimia 100, ujenzi wa jengo la malori asilimia 80, Ghala asilimia 85, jengo la mifugo asilimia 84, jengo la abiria asilimia 81, geti namba 1&2 asilimia 75 na mizani asilimia 85.

Mhandisi Mandari ameongeza kuwa mkandarasi amekwishakamilisha kazi za uandaaji wa ushindiliaji matuta ya karibu barabara zote na kwa sasa anendelea kukamilisha miundombinu ya mabomba ya maji safi, taka, zimamoto kabla ya kuanza tabaka la lami.
Kazi za ujenzi wa jengo la abiria katika Kituo cha Pamoja Mpakani (OSBP) eneo la Kasumulu/ Songwe mpakani mwa Tanzania na Malawi zikiendelea.

Kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha huduma ya pamoja mpakani (OSBP) mpakani mwa Tanzania na Malawi katika eneo la Kasumulu kutakuza uchumi wa nchi zote mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news