Wanafunzi waliotekwa nyara na kuachiwa huru waungana na familia zao

ABUJA, Wanafunzi 15 wameungana tena na familia zao wiki saba baada ya kutekwa nyara kutoka shule yao iliyopo Kaskazini Magharibi mwa Nigeria. Mwanafunzi aliyekuwa ametekwa na kuachiwa huru akiungana na familia yake katika Shule ya Sekondari ya Bethel Baptist huko Damishi nchini Nigeria. (Picha na AP).

Kwa mujibu wa VOA, mzazi mmoja anasema, baadhi ya wanafunzi hao wako hospitali kwa matibabu baada ya kukumbwa na madhila hayo.

Kwa ujumla wanafunzi 121 walitekwa nyara kutoka shule ya sekondari ya Bethel Baptist katika jimbo la Kaduna na polisi wanasema juhudi zinaendelea kuwatafuta wanafunzi 65 ambao bado wanashikiliwa.

Kiongozi mmoja wa mji anasema, fidia imetolewa ili kuachiliwa kwa wanafunzi lakini watekaji nyara wamewaachilia wachache kuliko idadi walioahidi.

Maafisa wa usalama wa Nigeria wameshiundwa kuzuia utekaji wa halaiki unaonedelea nchini humo zaidi ya wanafunzi elfu moja wameshatekwa tangu Desemba, mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments