Waziri Mchengerwa atembelea kiwanja kitakachojengwa jengo kubwa la ofisi Mji wa Serikali Mtumba

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwasili kwenye kiwanja ambacho ofisi yake imemkabidhi Mkandarasi TBA na Mshauri Mwelekezi WHC kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo kubwa la ofisi yake kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Waliombatana nae ni Katibu Mkuu wa ofisi yake, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia kwake) na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Francis Michael (kushoto kwake).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa maelekezo ya ujenzi wa wa jengo kubwa la ofisi yake kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Wanaopokea maelekezo hayo ni Katibu Mkuu wa ofisi yake, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Francis Michael (kushoto kwake) na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa ofisi yake Bw. Musa Magufuli (kulia kwake).
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo kubwa la Ofisi ya Rais-UTUMISHI litakalojengwa kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (mwenye barakoa). Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Francis Michael (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw. Musa Magufuli (kulia kwa Mhe. Waziri).
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (wa kwanza kulia) akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (mwenye barakoa) mipaka ya kiwanja ambapo Ofisi ya Rais-UTUMISHI itajenga jengo kubwa la ofisi kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia kwa Mhe. Waziri) na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Musa Magufuli (wa kwanza kushoto. (Picha zote na James K. Mwanamyoto-Ofisi ya Rais-UTUMISHI).

Post a Comment

0 Comments