TRA YAFAFANUA ANAYETAKIWA KULIPA KODI MPYA YA MAJENGO KUPITIA LUKU

NA MWANDISHI MAALUM

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.
Hayo yameeleza na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.

“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata bili mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.

Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.

Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.

Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 6,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 5,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 6,000.

Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news