ZANACO FC yawalaza Yanga SC kwa machozi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wiki ya Wananchi kwa mashabiki wa klabu ya Yanga imefikia tamati leo.

Ambapo sherehe hiyo imefanyika mkoani Dar es Salaam huku wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya ZANACO FC ya nchini Zambia ambapo wamefungwa mabao 2-1 licha ya kipindi cha kwanza kuongoza.
Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Heritier Makambo ndiye alianza kupachika bao dakika ya 30.

Ni baadaye kipindi cha pili Hakim Mniba na la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dakika 77.

Kocha Mkuu wa ZANACO FC, Kelvin Kaindu amesema kuwa, mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.

Kilele cha Wiki ya Wananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutN

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wakubwa Serikalini akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ambaye alipata fursa kuzungumza na mashabiki katika hafla hiyo.

Akitoa salamu zake mgeni rasmi katika kilele hicho Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amewataka wanachama na wapenzi wa timu hiyo kuzidi kushikamana na kushirkiana ili kuendelea kuikuza timu hiyo.

Amesema ni vyema kwa viongozi wa timu wakashikamana kwa pamoja kutatua chanagmoto mbalimbali zinazowakabili kwa lengo la kuendeleza uhai wa Klabu hiyo Kongwe nchini Tanzania.

Amesema Serikali zote mbili ile Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi zinaunga mkono jitihada zinazochukuliwa na timu za michezo mbalimbali ambapo viongozi hao wameahidi kukuza michezo nchini.

Akigusia suala la nidhamu, Mheshimiwa Hemed amewaasa wanachama na wachezaji wa timu ya Yanga kudumisha nidhamu wakiwa ndani na nje ya mchezo ili kuijengea heshima timu hiyo na taifa kwa ujumla.Katika kilele hicho, Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara ameweza kuwatambulisha wachezaji watakaochezea timu hiyo, ambao wamesajiliwa kisheria kwa kupeperusha bendera ya timu hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news