Wizara ya Habari, Utamadun, Sanaa na Michezo imeagiza shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha mfumo wa (VAR -Video Assistant Referee) unafungwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na Uwanja wa Arusha mara baada ya kukamilika.
Hatua hiyo inalenga kupunguza malalamiko na changamoto zinazojitokeza katika maamuzi ya marefa wakati wa michezo, pamoja na kuongeza uwazi na haki katika mashindano na kuimarisha usimamizi wa michezo kuendana na viwango vya kimataifa katika uendeshaji wa mashindano ya soka.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




















