ZOEZI LA UTOAJI WA KINGA TIBA ZA MABUSHA, MATENDE NA MINYOO YA TUMBO MTWARA MIKINDANI

NA MWANDISHI MAALUM

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko anapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa kuanzia tarehe 29/08/2021 hadi tarehe 04/09/2021Manispaa inaendesha zoezi la Utoaji wa Kinga tiba za Matende, Mabusha na Minyoo ya tumbo kwa Wananchi wote wenye umri unaoanzia miaka mitano na watu wazima wote.
Zoezi hili linafanyika kwa siku Saba na litafanywa na wagawa dawa ambao watapita nyumba kwa Nyumba Kutoa Kinga tiba hizo.

Ili kufanikisha zoezi hili Wananchi wote mnaombwa kutoa ushirikiano kwa wagawa dawa pindi watakapokuwa wanapita kwenye nyumba zenu.

Ikumbukwe kuwa Kinga ni Bora kuliko Tiba hivyo ni vema kila mmoja akahakikisha anapata Kinga tiba kwa Ustawi wa maisha yake ya Sasa na ya baadae.

Imetolewa na:-

Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Mtwara-Mikindani


30/08/2021.

Post a Comment

0 Comments