Baba mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kambo wa miaka sita

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

JESHI la polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi wa Kata ya Dutwa, Nduru Ndazi (49) kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita ambaye ni mtoto wake wa kambo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao amesema, tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Majengo Kata ya Dutwa Wilaya ya Bariadi.

Amesema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kumnajisi mtoto huyo wa mkewe kwa tamaa ya kimapenzi.

Kamanda huyo amesema, mtuhumiwa huyo yuko mahabusu akisubiri kufikishwa mahakamani.

Pia ametoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya ukatili na kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Bariadi, Lilian Mishita amesema,mtoto huyo baada ya kufikishwa hospitali na kufanyiwa vipimo katika hospitali ya wilaya ya Dutwa ilibainika kuwa ni kweli alifanyiwa kitendo hicho na inaonesha si mara moja kutendewa hivyo.

Post a Comment

0 Comments