BREAKING NEWS: Nabii Joshua anusurika kifo katika ajali 'Asante Mungu haujaniacha niangamie'

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KIONGOZI Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Joshua Aram Mwantyala amenusurika kifo katika ajali mbaya akielekea katika Operesheni Ombeni Bila Kukoma huko Ifakara mkoani Morogoro.



Nabii Joshua ambaye Mungu amempa karama ya kipekee katika kuomba na kuhubiri neno la Mungu, siku za karibuni alitangaza operesheni hiyo ambayo imedhamiria kutoa dozi ya tiba kwa magonjwa yote yanayowatatiza Watanzania yakiwemo ya upumuaji katika mfumo wa hewa, kuokoa waliofungwa katika vifungo vya giza, kurejesha uchumi uliopigwa na shetani na mengine mengi.
"Leo tumepita mautini baada ya gari langu kuanguka Mungu, amekataa kuniacha niangamie jina lake litukuzwe.Imeandikwa, mwenye haki wangu hupatikana na mabaya mengi, lakini Bwana humshindia na hayo yote,"ameeleza Nabii Joshua baada ya Mungu kumuokoa katika ajali hiyo mbaya.

Pia hivi karibuni akiwa makao makuu ya Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania yaliyopo Yespa, Kihonda mjini Morogoro wakati akizungumzia juu ya operesheni hiyo ambayo itafanyika mfululizo ili kumweleza Mungu hitaji la Watanzania kwa sasa, Nabii Joshua amesema, operesheni hiyo inaenda sambamba na ile ya Ombea Taifa (Pray for Nation) ambayo aliiasisi miaka kadhaa iliyopita na imeleta mafanikio makubwa katika Taifa ikiwemo kuwaponya maelfu ya Watanzania.

“Tunakwenda kuongozwa na neno la Mungu kutoka 1 Wathesalonike 5:17, Biblia inaeleza kuwa, “ombeni bila kukoma”. Nasi tunakwenda kuomba bila kukoma ili Mungu wetu ambaye ndiye muumba Mbingu na nchi aweze kutuondolea changamoto zote za kiafya na mambo mengine yanayotukabili kwa sasa na hakika Mungu anakwenda kujibu maombi yetu,”amesema Nabii Joshua.

Wakati huo huo, Nabii Joshua ametoa wito kwa Watanzania wote bila kujali dini, makabila au vyeo vyao kujinyenyekeza mbele za Mungu, kwani akiwa katika maombi Roho Mtakatifu amekuwa akimsisitiza kuyasema hayo kwa kuwa, roho za giza na mauti zinaendelea kulinyemelea Taifa na watu wake.

"Tuombe... Tuombe....Tuombe wana wa Mungu, vita iliyopo kwa sasa katika ulimwengu wa kiroho ni hatari sana, tufanye maombi kwa ajili ya Taifa letu, viongozi wetu chini ya mama yetu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, na tuzikabidhi familia zetu kila dakika katika maombi, na hakika tutayashinda yote kwa jina la Yesu Kristo,"ameongeza Nabii Joshua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news