Biashara United yazamisha jahazi la Dikhili FC, yawatandika 2-0

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Timu ya Biashara United kutoka mkoani Mara imetinga hatua ya awali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dikhili FC.
Ramadhan Chombo (Redondo) ndiye aliyezamisha jahazi la Dikhili FC.

Mtanange huo umepigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Ndoto za wageni zilizimwa katika dakika ya 19 na 23 ambapo Redodo aliharibu mipango yao.

Pia alikosa penalti dakika ya 27 ambayo ingemfanya aweze kuondoka na mpira wake kwa kufunga hat trick katika mtanange huo safi.

Awali wakiwa ugenini Biashara United ilishinda kwa bao 1-0 hivyo jumla inasonga mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.

Post a Comment

0 Comments