Bima ya Afya kwa Wote kuwa mkombozi kwa Watanzania-Waziri Mkuu

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema muswada wa Bima ya Afya kwa wote utakapokamilika utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa Watanzania kwani utakwenda kufanikisha mkakati wa Serikali wa kuwapatia watanzania huduma bora za afya.

Amesema, Serikali inaendelea kufanya maboresho makubwa ya ujenzi wa miundombinu ya afya, zikiwemo hospitali pamoja na vifaa tiba, hii ikiwa ni dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na zenye uhakika.

“Serikali inaimarisha upatikanaji wa bidhaa za Afya nchini ikiwa ni pamoja na dawa, vifaa tiba na kuanzia mwezi Juni, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 31 kwa ajili ya kuhakikisha vifaa hivyo vinapatikana hivyo nataka niwahakikishie watanzania kuwa Serikali itaendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa na huduma bora za afya nchini; 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa wakiongoza mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon) zilizoanzia katika viwanja vya Leaders Club kupitia Oystarbey jijini Dar es Salaam, Septemba 25, 2021. Wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCRBT, Brenda Msangi na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna.

Waziri Mkuu Ameyasema hayo leo Septemba 25, 2021 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kushiriki mbio za hisani zilizoandaliwa na benki ya NMB.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeanza ujenzi wa kiwanda kwa ajili ya uzalishaji wa ‘Gloves’ na dawa aina tano zikiwemo vidonge, ‘syrup’, ‘Capsules’, kwa lengo la kukidhi mahitaji ya nchi.

“Kiwanda hicho kitasaidia kuokoa shilingi bilioni 33 ikilinganishwa na shilingi bilioni 54 kwa mwaka ambazo zinatumika kununua bidhaa za afya sita zitakazozalishwa kiwandani hapo,"amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mazoezi ya viungo baada ya kumalizi mbio za Hisani Benki ya NMB (NMB Marathon 21) zilizoanzia kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam kupitia Oysterbay na kuishia kwenye viwanja hivyo, Septemba 25, 2021. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala, wa pili. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhende na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kumaliza mbio za kilomita 5 zilizoanzia Viwanja via Leaders kupitia Oysterbay na baadae kurejea Leaders Club jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivishwa medali ya ushindi wa mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon 2021) na Mwenyekiti wa Benki hiyo, Dkt. Edwin Mhende baada ya kumaliza mbio hizo zilizoanzia Viwanja vya Leaders Club kupitia Oysterbay na kuishia kwenye viwanja hivyo jijijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi milioni 400, 000,000/= , Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi (aliyenyosaha mkono) baaada kumalizika kwa mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon 21) zilizoanzia kwenye viwanda vya Leaders Club kupitia Oysterbay jijini Der es salaam, Septemba 25, 2021. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mwenyekti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB, Dkt.. Edwin Mhenda na Kulia ni Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Aidha, Waziri Mkuu ametoa pongezi kwa benki ya NMB na CCBRT kwa pamoja na wadau wengine kwa namna wanavyounga mkono Serikali katika kuwahudumua kinamama wanaopata ugonjwa wa Fistula.

Naye, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano wanawake zaidi ya elfu tano miatano wameshatibiwa ugonjwa wa fistula na asilimia kubwa wametibiwa katika Hospitali ya CCBRT.

“Hii inatokana na kampeni ya inayoendeshwa kati ya Serikali na wadau ambao kuna mabalozi zaidi ya 3000 nchi nzima kushughulikia wagonjwa wa fistula na kuwapeleka katika hospital zinazotoa huduma za fistula,"amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema kuwa lengo la mbio hizo zilikuwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula.

Zaipuna amesema kuwa, kupitia mbio hizo za hisani wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 400 ambao zitaweza kutoa matibabu kwa kinamama 100 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news