Mambo manne yaliyobeba Kitabu cha Rai ya Jenerali


Na Blandina Aristides, Mwanza

Kitabu cha Rai ya Jenerali kimebeba mambo makuu manne ambayo ni: 1. Haja ya Kuheshimu Hoja 2. Haja ya kuheshimu maoni 3. Haja ya mabadiliko kila wakati 4. Haja ya uhuru kama msingi wa maendeleo

Imeelezwa kuwa moja ya mambo makuu muhimu yaliyobeba Kitabu cha Rai ya Jenerali ni pamoja na Haja ya Kuheshimu Hoja.

Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza, Askofu Benson Bagonza ameeleza kuwa hoja hiyo inatoa fursa ya kuheshimu hoja za watu na si kupiga kelele.

"Kuna watu wengi wanapiga kelele tu, lakini wanachokizungumza hakieleweki,"alisema Bagonza.

Aliyataja mambo mengine yanayobeba kitabu hicho kuwa ni pamoja na haja ya mabadiliko kila wakati, haja ya kuheshimu maoni,na haja ya uhuru kama msingi wa maendeleo ambavyo ni utu, lakini pia ni uhuru.

Kitabu hicho kimeandikwa na mmoja wa waandishi wa habari wakongwe nchini Jenerali Ulimwengu ili kuona hali ya nchi ilivyo tangu mwaka 1996 mpaka sasa.

Ulimwengu anasema,kitabu hicho kimebeba Makala na Mahojiano aliyoandika mwaka 1996 katika gazeti la Rai mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania.

Anasem, mambo mengi yaliyomo ndani ya Kitabu yanaeleza yaliyojiri mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa Rais na wabunge kutoka vyama mbalimbali na yeye akiwa mmoja wa wagombea.

Post a Comment

0 Comments