Mhandisi Sanga akagua utendaji kazi wa Sekta ya Maji Mtwara

NA MWANDISHI MAALUM

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga mwishoni mwa wiki amekagua utendaji wa Sekta ya Maji mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akikagua chanzo cha maji cha Mbwinji kinachotumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi Nachingwea (MANAWASA) kusambaza huduma ya maji, (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa MANAWASA Mhandisi Nuntufye Mwamsojo
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelekezo ya kitaalamu kuhusu ujenzi unaoendelea wa mradi wa maji wa Chipingu, pamoja naye (katikati) ni Mbunge wa Lulindi Mhe. Issa Ally (Mb) na wataalamu wa sekta ya maji. Chanzo cha maji cha mradi huo ni mto Ruvuma.

Mhandisi Sanga katika ziara hiyo ya kikazi amewataka watendaji na wataalamu wa sekta ya maji kutumia ubunifu katika kutoa huduma, na kuepuka gharama ambazo hazina ulazima.

Amesisitiza wataalamu kutumia usanifu wa miradi utakaowezesha majisafi kuwafikia wananchi kwa njia ya mserereko, hivyo huduma hiyo kumfikia mlaji kwa gharama ndogo.

Post a Comment

0 Comments