Mwinjilisti Alphonce Temba arejea nchini kwa kishindo,akomboa ardhi, nyumba zilizofungwa kishirikina Tunduma

NA MWANDISHI DIRAMAKINI
 
Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba amerejea nchini kutoka katika ziara ya uinjilisti wa Kimataifa katika mataifa ya Zambia na Botswana
 
Temba ndiye aliyetabiri kuhusu ushindi wa Chama cha Upinzani cha United Party for National Development (UPND) nchini Zambia katika uchaguzi wa hivi karibuni.
 
Baada ya kuingia nchini Muhubiri na Mwinjilisti wa kimataifa Alphonce Temba huku akiwa amebeba upako wa Wafalme kwa nchi ya Botswana na Zambia, Roho Mtakatifu alimuongoza kwenda kufanya operesheni maalum ya ukombozi wa ardhi mjini Tunduma.
 
Ukombozi wa aridhi ulianzia Chapwa mjini Tunduma ndani ya aridhi ya nyumba zilizokuwa zikiombewa wafanyakazi wajenzi walianza kuangushwa na nguvu za Mungu zisizo za kawaida na kufunguliwa.
 
"Leo hii mji wa Tunduma umekuwa na nyumba nyingi ambazo kabla hazijaisha ama wenye nyumba wanakufa au wanaishia kuwa mapagana na kuuzwa zingine. Wakati maombi yanaendelea jirani mmoja alikuja mbio eneo husika na kuanza kupiga kelele nakuomba radhi bila kusema jambo gani, hata hivyo aliuliza mmoja wa mwanafamilia kuwa amekuja hapo, jambo ambalo limemuacha mdomo wazi hata hivyo jirani huyo inayesemekana ana vitendo vya ushirikina, alishindwa kutulia akatoweka eneo hilo huku akiwa na hofu baada ya kuwaona mafundi wakiwa wameanguka ovyo.
 
"Ni baada ya kuangushwa na nguvu za Mungu kila aridhi kuna sauti inapiga kelele,"amefafanua Mwinjilisti Temba.  Je? Sauti gani inapiga kelele katika nyumba yako kutana na mpakwa mafuta wa Bwana nyumba yako ikombolewe Mtumishi Alphonce Temba wasiliana naye kupitia simu +255755973787.
Kundi kubwa la watu ambao walisemekana wanatumia nguvu za giza, baadae walifika eneo hilo wakitetemeka.
 
Aidha, Mwinjilisti Temba amesema kuwa, kusudi Mungu aliloweka ndani yake la kufungua nira zote za yule adui muovu shetani, limemsukuma kuufungua mji wa Tunduma ambalo ni moja ya eneo lililopo mpakani mwa Tanzania na Zambia lenye idadi kubwa ya wafanyabiashara.
 
Amesema, eneo hilo lisipofunguliwa kwa maombi wachawi watatamba mitaani, huku ikijulikana wazi kuwa, wananchi wengi wanalitumia eneo hilo kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
 
Kwani Tunduma ndio mpaka mkubwa zaidi ya mipaka yote kuachilia Bandari ya Dar es Salam unakadiriwa mzunguko wa uchumi wa mali zinazopita kwa siku ni zaidi ya tirioni moja kwenda nchi za Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Namibia, Congo DRC na Afrika Kusini, hivyo watu wanautajiri mkubwa na mzunguko mkubwa wa fedha kutokana na shuguli za kibiashara kama za mazao, mbao na kadhalika.
 
Vijana wengi wamejiajiri katika biashara nyingi ikiwemo za kubadilisha fedha ambapo kijana mmoja anaweza kuwa na zaidi ya dola elfu kumi kwa kubadilisha na fedha za mataifa yote ya jirani kama Malawi, Zambia, Afrika Kusini na Tanzania.
 
Kutokana na mashindano makubwa ya kibiashara imani za kishirikina zimekuwa zikipata nafasi kubwa sana na hata katika ujenzi wa nyumba hasa za kibiashara, kwani watu wengi wanaishia kufa na kushindwa kumalizia miradi yao.
 
Ndiyo maana Roho wa Mungu akamwongoza mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Temba kukomboa aridhi ya Tanzania katika nguvu za giza, matambiko ya uchawi, ushirikina wa mazingaombwe.
 
Pia mila za maagano, desturi vijicho, uloz,i kafara, misukule, madhabau wanga, tego na nguvu za ukoo na mila toka kwa wazee wa pande zote za wazazi pande zote za mababu na mabibi.
 
"Kwani pamoja na huduma za kiroho zilizopo Mbeya na Tunduma ambazo ni nyingi kuliko zilizopo kote nchini bado aridhi inahitaji kukombolewa kwa sauti za hayo makafara yanayopiga kelele, Mwanzo 4.9-10.
 
"Pia kununuliwa kwa kuhitaji ukombozi wa Damu ya Yesu, hivyo moto umewaka na utaendelea nchi nzima akikisha unakombolewa katika eneo lako kama neno llisemavyo katika kitabu cha Joshua 1.3 hili watu wa Mungu wawe huru,"amesema Mwinjilisti Temba.

Post a Comment

0 Comments